Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mvinyo Unaolevya

  Divai ambayo Kristo aliifanyia kwa maji katika karamu ya arusi ya Kama ilikuwa majimaji matupu ya zabibu. Hii ni “divai mpya ipatikanavyo katika kichala,” ambacho Biblia yasema, “Usikiharibu kwa maana mna baraka ndani yake” (Isaya 65:8).KN 118.4

  “Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi;
  Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”
  “Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
  Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.”
  “Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole?
  Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno?
  Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu?
  Ni nani aliye na macho mekundu?
  Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo;
  Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
  Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
  Litiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;
  Mwisho wake huuma kama nyoka;
  Huchoma kama fira”.
  KN 118.5

  (Mithali 20:1; 23:29-32).

  Maneno haya yanaeleza mfano halisi wa uharibifu na utumwa unaompata mtu kwa sababu ya ulevi, kwa namna asivyoweza mwanadamu awaye yote kuuelezea. Ulevi unamtia mtu utumwani, unamwondolea heshima, na hata akijulishwa hali yake jinsi ilivyo mbaya sana, hawezi kujitoa katika tanzi; atazidi “kuitafuta tena” (Mithali 23:35).KN 119.1

  Mvinyo, pombe, na kinywaji kinachotengenezwa kwa kusindika matofaa hulevya kama vile vileo vilivyo vikali zaidi. Kutumia vileo hivi kunaamsha kiu ya kutaka kuvipata vile vilivyo vikali zaidi, ndivyo mazoea mabaya ya ulevi wa pombe yanavyoanza. Kunywa vileo kwa kiasi ni shule ambapo watu hufundishwa kuwa na maisha ya mlevi. Ingawa kazi ya vileo hivi visivyo vikali ni ya pole pole, lakini ni njia kuu ya kuingilia ulevini kabla mtu hajadhania hatari yake.KN 119.2

  Hakuna haja ya kutumia maneno mengi ili kuthibitisha ubaya wa matokeo ya ulevi. Wenye macho mekundu, wenye kupumbaa wanaoangamia kwa kunywa ulevi mwingi-watu ambao pia Yesu Kristo aliwafia, na ambao malaika huwalilia-wako kila mahali. Wanatia fedheha ustaarabu wa watu tunaojivunia. Wao ni aibu na balaa na hatari ya kila nchi. 7MH 330-333;KN 119.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents