Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Kutayarisha Njia

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 10 - Imani kwa Mungu Aliye Hai

  ITAONEKANA siku ya kukata maneno mara ya mwisho kuwa Mungu alijua jina la kila mmoja. Kuna shahidi asiyeonekana kwa kila tendo la maisha. “Nayajua matendo yako” ndivyo asemavyo “yeye aendaye katikati ya vinara saba vya dhahabu.” (Ufunuo 2:1). Imejulikana nafasi zilizodharauliwa, jinsi Mchungaji Mwema alivyofanya bidii bila kulegea kuwatafuta wale ambao wamepotea katika njia zilizopotoka, na kuwarudisha kwenye njia ya salama na amani. Mara kwa mara amemulika nuru ya Neno njiani mwao, ili wapate kuona hatari yao, na kuepuka. Lakini wamezidi kuendelea, wakifanya mzaha na kudhihaki wakisafiri katika njia pana, mpaka mwishowe muda wao wa kuangaliwa kama wanafaa au nawafai uishe. Njia za Mungu ni za haki na sawa; na hukumu itakapotolewa juu ya wale wanaoonekana wamepungua, kila kinywa kitafumbwa. 1.KN 86.1

  Mungu ni roho; lakini ni nafsi, maana mtu aliumbwa kwa sura yake. Kazi ya mikono ya Mungu kwenye viumbe si Mungu mwenyewe. Viumbe vya asili ni ufunuo wa tabia ya Mungu; kwa njia ya viumbe hivyo twaweza kuufahamu upendo wake, uwezo wake, na utukufu wake; lakini haitupasi kuvihesabu viumbe kama ni Mungu. Akili ya kazi ya sanaa ya wanadamu hutoa ustadi mzuri ajabu, vitu vinavyopendeza macho, na vitu hivi hutupa sisi wazo fulani la fundi huyo wa sanaa; lakini kitu kilichofanywa si mtu. Siyo kazi, bali fundi ndiye mwenye kustahili sifa. Hivyo, huku viumbe vikiwa ufunuo wa mawazo ya Mungu, siyo viumbe bali Mungu aliyeviumba ambaye hupaswa kutukuzwa.KN 86.2

  Katika kumwumba mtu nguvu za Mungu wa pekee zilidhihirishwa. Wakati Mungu alipokuwa amemwumba mtu kwa sura yake, umbo la binadamu lilikuwa kamili katika maumbile yake yote, lakini halikuwa na uhai. Kisha Mungu wa pekee, asiye na mwanzo wala mwisho ambaye hakuumbwa akalipuiizia lile umbo pumzi ya uhai, na mtu akawa nafsi hai, mwenye kupumua, mwenye akili. Viungo vyote vya mwili wa binadamu vikafanya kazi. Moyo, ateri, vena, ulimi, mikono, miguu, akili, ufahamu wa ubongo-vyote vikaanza kazi yao, na vyote viliwekwa chini ya sheria. Mtu akawa nafsi hai. Kwa njia ya Yesu Kristo Mungu wa pekee alimwumba mtu na kumjalia akili na uwezo.KN 86.3

  Mwili wetu haukufichika kwake tulipoumbwa kwa siri. Macho yaliona mwili wetu, ijapokuwa si kamili; na kitabuni mwake viungo vyetu vya mwili viliandikwa, kabla havijakuwako hata kimoja.KN 86.4

  Zaidi ya viumbe vyote duniani, Mungu alikusudia kuwa binadamu, aliye kazi bora zaidi ya uumbaji wa Mungu apaswa kuonyesha mawazo ya Mungu na kufunua utukufu wake. Lakini binadamu asijitukuze mwenyewe kama Mungu. 28T263-273KN 87.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents