Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Kutayarisha Njia - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushirika

    Katika kuanzisha taasisi za kazi mahali papya mara nyingi hulazimu kuweka kazi za madaraka kwa watu ambao hawaielewi kazi hii kinagaubaga. Watu hawa hufanya kazi na kuleta hasara kubwa, na kama wao na watenda kazi wenzao hawatakuwa na moyo wa kufikiri wengine kuliko nafsi zao wenyewe katika kazi ya Mungu, patakuwako matokeo ya hali ya mambo ambayo yatazuia mafanikio yake.KN 52.4

    Wengi huona kuwa aina ya kazi wanayoifanya ni yao wenyewe na ya kuwa hakuna mtu mwingine apaswaye kutoa shauri lolote kuhusu uboreshaji wa utendaji wao. Yawezekana watu hawa wakawa hawana uelewa kabisa juu ya kazi yao, lakini kama mtu akithubutu kuwapa shauri jema, hukasirika na kunuia kufuata waonavyo wao wenyewe. Tena, watenda kazi wengine hawakubali kusaidia au kuwafundisha watenda kazi wenzao. Wengine wasio na uzoefu hawataki kutokujua kwao kujulikane. Wanafanya makosa, wakipoteza wakati mwingi na vifaa, kwa sababu wanajivuna sana kiasi kwamba hawawezi kutaka shauri kwa mwingine.KN 52.5

    Asili ya shida hii sio jambo gumu kuligundua. Watenda kazi wamekuwa nyuzi zinazojitegemea, wakati ambapo wanapaswa kujihesabu kama nyuzi ambazo hazina budi kusokotwa pamoja kusaidia kufanya kielelezo.KN 52.6

    Mambo haya humhuzunisha Roho Mtakatifu. Mungu anataka kila mmoja awe radhi kujifunza toka kwa mwenzake. Kujitegemea kusiko safi hutuweka mahali ambapo Mungu hawezi kufanya kazi pamoja nasi. Hali ya mambo ikiwa hivi Shetani hupendezwa sana.KN 53.1

    Kila mtenda kazi atapimwa ili kuona kama utendaji wake ni kwa manufaa ya kazi ya Mungu, au kwa kujinufaisha mwenyewe.KN 53.2

    Dhambi ambayo karibia hakuna matumaini ya kuiondoa na inakaribia kabisa kutotibika ni kiburi cha mawazo na majivuno. Hii huzuia ukuaji wote. Mtu akiwa na kasoro kitabia, lakini akakosa kulifahamu jambo hili; akiwa amejawa na kujitosheleza kiasi kwamba hawezi kuona makosa yake atawezaje kusaflshwa? “Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi” (Mathayo 9:12). Mtu anawezaje mtu kuboresha hali yake ya kiroho wakati anadhani kuwa njia zake ni kamilifu?KN 53.3

    Mkristo mwenye moyo mkamilifu ndiye tu anayeweza kuwa mwungwana halisi. 77T 197 - 200].KN 53.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents