Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kosa Baya

    Kosa kubwa lililosababisha mabaya haya kwa Ufaransa ilikuwa ni kupuuza ukweli huu mkuu: kwamba uhuru wa kweli uko kwenye uzingatiaji wa makatazo yaliyobainishwa katika sheria ya Mungu. “Laiti ungasikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari.” Isaya 48:18. Wale ambao hawatajifunza kutoka katika Kitabu cha Mungu wanapaswa kukisoma kupitia histona.TK 184.2

    Shetani alipolitumia Kanisa la Roma kuwapotosha watu wasitii, kazi yake ilikuwa inafanywa kwa hila. Kutokana na utendaji wa Roho wa Mungu makusudio ya Shetani yalizuiliwa yasikomae na kuzaa matunda. Watu hawakufuatilia matokeo ya tendo na kugundua chanzo cha masumbuko yao. Lakini wakati wa Mapinduzi Baraza la Taifa liliiweka kando sheria ya Mungu. Na kwenye Enzi ya Hofu kuu iliyofuata, athari za tendo na matokeo zingeonekana kwa watu wote.TK 184.3

    Kuvunjwa kwa sheria njema na ya haki ya Mungu kungeleta uharibifiu. Roho wa Mungu azuiaye na kudhibiti nguvu za ukatili wa Shetani, kwa kiwango kikubwa alikuwa ameondolewa, na yule anayependelea kuona wanadamu wakiwa kwenye hali mbaya aliachwa kutenda kazi. Waliokuwa wamechagua uasi waliachwa kuvuna matunda yake. Nchi ilikuwa imejaa uhalifu. Kutoka kwenye mikoa iliyoharibiwa na miji iliyokuwa imeangamia kilio cha kuogofya kilisikika kwa maumivu na uchungu mkuu. Ufaransa ilikuwa imetikiswa kwa mfano wa tetemeko la nchi. Dini, sheria, utaratibu wa kijamii, familia, taifa na kanisa - vyote vilikuwa vimeangushwa na mikono ya udhalimu iliyokuwa imeinuliwa kinyume cha sheria ya Mungu.TK 184.4

    Mashahidi waaminifu wa Mungu walikuwa wamechinjwa na utawala wa “mnyama atokaye katika kuzimu,” wasingeendelea kunyamaza kwa muda mrefu. “Na baada ya siku hizo tatu u nusu, roho ya uhai itokayo kwa Mungu ikawaingia, wakasimama juu ya miguu yao; na hofu kuu ikawaangukia watu waliowatazama.” Ufunuo 11:11. Mwaka 1793 amri zilitolewa kutoka katika Bunge la Ufaransa kupiga marufuku Biblia. Miaka mitatu na nusu baadaye, azimio la kutangua maagizo hayo lilikubaliwa na baraza hilohilo. Wanadamu walikuwa wamegundua umuhimu wa imani kwa Mungu na Neno lake kama msingi wa utu wema na uadilifu.TK 185.1

    Kuhusiana na “mashahidi wawili”[Agano la Kale na Jipya] nabii anaendelea kusema: “Wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, Pandeni hata huku. Wakapanda mbinguni katika wingu, adui zao wakiwatazama.” Ufunuo 11:12. “Mashahidi wawili wa Mungu” wametukuzwa sana kuliko ilivyokuwa hapo awali. Mwaka 1804 Shirika la Biblia la Uingereza na Nchi za Nje lilianzishwa, likifuatiwa na mashirika mengine ya aina hiyo barani Ulaya. Mwaka 1816 shirika la Biblia la Amerika lilianzishwa. Tangu wakati huo Biblia imetafsiriwa katika mamia ya lugha. (Angalia Kiambatisho.)TK 185.2

    Kabla ya mwaka 1792 kazi ya utume katika nchi za nje ilikuwa imepewa uzito kidogo. Lakini kuelekea mwisho wa kame ya kumi na nane mabadiliko makubwa yalitokea. Watu hawakuridhika na falsafa ya mantiki na walitambua umuhimu wa ufunuo wa Mungu na dini ya vitendo. Kuanzia wakati huu vituo vya kimisionari nchi za nje vilifikia ukuaji ambao haukuwepo hapo kabla.(Angalia Kiambatisho).TK 185.3

    Maendeleo katika taaluma ya uchapishaaji yameleta msukumo katika usambazaji wa Biblia. Kusambaratika kwa hisia za kale, ubaguzi wa utaifa, na kupotea kwa nguvu za utawala wa Papa wa Roma; kumefungua njia kwa ajili ya Neno la Mungu. Kwa sasa Biblia imepelekwa kila mahali duniani.TK 185.4

    Mkanamungu Voltaire alisema: “Nimechoshwa na watu wanaorudia rudia kusema, watu kumi na wawili walianzisha dini ya Kikristo. Nataka kuwathibitishia kwamba mtu mmoja anatosha kuiangusha.” Mamilioni wamejiunga kuipiga vita Biblia. Lakini haiwezekani kuiharibu. Pale palipokuwa na Biblia mia moja wakati wa Voltaire, leo hii kuna nakala laki moja za Kitabu cha Mungu. Kwa kauli ya Mwanamatengenezo wa awali, “Biblia ni chuma anachopondea mhunzi ambacho kimechakaza nyundo nyingi.”TK 186.1

    Chochote kilichojengwa juu ya mamlaka ya mwanadamu kitaangushwa, na kile kilichojengwa juu ya mwamba wa Neno la Mungu, kitasimama milele.TK 186.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents