Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maridhiano na Makubaliano

  Waprotestanti wamekuwa wateja wa utawala wa utawala wa Papa; wamefanya maridhiano na makubaliano ambayo Wakatoliki wenyewe wanashangaa kuyaona. Wanadamu wanaifumbia macho tabia halisi ya Ukatoliki. Watu wanatakiwa kuzipinga hatua za huyu adui hatari kuelekea kwenye uhuru wa kiraia na uhuru wa kidini.TK 344.2

  Wakati Ukatoliki umejengwa juu ya udanganyifu, haimaanishi kuwa ni mfumo duni usio na ustadi. Huduma ya ibada ya Kanisa la Roma ni ya kuvutia sana. Mwonekano wake wenye mapambo ya kufurahisha na ibada yenye kicho inawapumbaza watu na kunyamazisha uwezo wa kuangalia mantiki na dhamiri. Jicho linavutwa. Makanisa yanayovutia, maandamano ya ibada, mimbara za dhahabu, vihekalu vyenye nakshi za vito, picha zilizochorwa kwa ustadi na sanaa zenye ubora zinavutia kupenda uzuri. Muziki hauna mpinzani. Muziki mwanana unaopigwa kwa mpangilio mzuri na mchanganyiko wa mawimbi ya sauti nyingi zinazopaa kwenye mahekalu makubwa na mazuri, unachochea moyo kuwa na kicho na heshima kubwa.TK 344.3

  Uzuri huu wa nje na sherehe haukidhi tamaa ya mtu mwenye kulemewa na dhambi. Dini ya Kristo haihitaji vivutio vya aina hiyo. Nuru ing’aayo kutoka kwenye msalaba inaonekana kuwa safi na iliyojaa upendo kiasi kwamba hakuna mapambo ya nje yawezayo kuongeza thamani yake ya kweli.TK 344.4

  Fikra za juu za kazi za sanaa, ulaini halisi wa ladha, mara nyingi vimetumiwa na Shetani kuwaongoza wanadamu kuyasahau mahitaji ya muhimu ya moyo na kuishi kwa ajili ya ulimwengu huu pekee.TK 344.5

  Fahari na taratibu za ibada za Kikatoliki zina nguvu ya kushawishi na kupumbaza, ambayo imewadanganya wengi. Wanaona kana kwamba Kanisa Katoliki ni lango la kuingilia mbinguni. Ni wale tu wanaokita miguu yao juu ya msingi wa ukweli, mioyo yao ikiwa imefanywa upya na Roho Mtakatifu, ambao hawataathiriwa na ushawishi wake. Mtindo wa maisha ya uadilifu bila nguvu zake ndiyo shauku ya watu wengi.TK 345.1

  Dai la kanisa kuwa na haki ya kusamehe dhambi linamfanya Mkatoliki kuhisi kuwa anao uhuru wa kutenda dhambi, ibada ya kitubio pia huchangia kuhalalisha uovu. Yule anayempigia magoti mwanadamu mwenye dhambi na kufunua katika maungamo mawazo ya siri za moyo wake anaivunjia heshima nafsi yake. Kwa kuzifunua dhambi za maisha yake kwa padre-mkosaji mwenye kupatwa na mauti - kiwango cha tabia yake kinashushwa, na matokeo yake ananajisika. Wazo lake kuhusu Mungu linashuka hadhi na kumfananisha na ubinadamu ulioanguka, maana padre anasimama kama mwakilishi wa Mungu. Maungamo haya yanayoshusha hadhi kati ya mwanadamu na mwanadamu, ni chemchemi ya siri ambayo kwayo kiasi kikubwa cha uovu unaounajisi ulimwengu unabubujika. Lakini kwa yeye apendaye kuiendekeza nafsi, inapendeza zaidi kuungama kwa mwanadamu mwenzake mwenye kupatwa na mauti kuliko kuufungua moyo wake kwa Mungu. Inakubalika zaidi kwa asili ya mwanadamu kutubu kuliko kuikana dhambi; ni rahisi kuudhalilisha mwili kwa nguo za magunia kuliko kuzisulubisha tamaa za mwili.TK 345.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents