Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 8 - Mtetezi Wa Ukweli

    Charles wa V, alipanda kwenye kiti cha ufalme wa Ujerumani. Mjumbe wa baraza la uchaguzi wa huko Saksoni ambaye kwa kiasi kikubwa alimsaidia sana Charles kuupata Ufalme wake; alimsihi kutomchukulia hatua yoyote Luther hadi atakapompa nafasi ya kusikiliza maelezo yake. FCwahiyo mfalme alitahayari na kupata mfadhaiko mkubwa. Wafuasi wa Kanisa la Roma wasingeridhika na jambo lolote zaidi ya kifo cha Luther. Mjumbe wa baraza la uchaguzi alikuwa ametangaza kuwa “Daktari Luther alipaswa kupewa ulinzi kwa ajili ya usalama wake ili aweze kusimama mbele ya mahakama ya wasomi, wacha Mungu, na majaji wasio na upendeleo” 64D’Aubigne, bk. 6, ch. 11.TK 94.1

    Mkutano ulifanyika katika mji wa Worms. Kwa mara ya kwanza wakuu wa Ujerumani walikuwa wanakutana na mtawala wao kijana kwenye kusanyiko. Watu wenye vyeo kanisani na serikalini na mabalozi wa nchi za kigeni wote walikusanyika katika mji wa Worms. Lakini jambo lililochochea mvuto mkubwa ni Mwanamatengenezo. Mfalme Charles alimwagiza Mjumbe wa baraza la uchaguzi kumleta Luther pamoja naye, alimhakikishia usalama na kuahidi kuwepo kwa majadiliano huru katika mambo yanayobishaniwa. Luther alimwandikia Mjumbe wa baraza la kura kwamba, “Kama mfalme ananiita, sina mashaka kuwa huo ni mwito wa Mungu mwenyewe. Kama wanatamani kutumia nguvu dhidi yangu,...ninaliweka jambo hili katika mikono ya Mungu...Endapo hataniokoa, maisha yangu yana umuhimu kidogo tu...Unaweza kutarajia kila kitu kutoka kwangu isipokuwa kukimbia na kubadili msimamo. Kukimbia sitaweza, na sitarudi nyuma.” 65Ibid., bk. 7, ch. 1.TK 94.2

    Kwa kadiri habari zilivyosambaa kwamba Luther angesimama mbele ya mkutano huo wa kimataifa, msisimko mkubwa ulichochewa. Aleander, balozi mdogo wa Papa alishtushwa na kughadhibishwa. Kuhoji kwenye shauri ambalo Papa alikwisha kulitolea tamko la hukumu ingekuwa ni kuidharau mamlaka ya baba mtakatifu. Zaidi ya hayo, hoja za mtu huyu zingeweza kuwageuza wengi wa wakuu hao wamwache Papa. Alimlalamikia Charles dhidi ya kusimamishwa kwa Luther huko Worms na alimshawishi mfalme kusalimu amri.TK 94.3

    Aleander hakuridhika na ushindi na akafanya bidii kuhakikisha kuwa Luther anahukumiwa. Alimtuhumu Mwanamatengenezo huyo kwa “uchochezi, uasi, utovu wa kicho, na mwenye kukufuru.” Lakini ukali wake ulifunua ni roho gani aliyekuwa anamchochea. “Alikuwa amesukumwa na hali ya chuki na kisasi,“ 66Ibid. hayo yalikuwa ndiyo maoni ya jumla. Aleander alitoa hoja kwa shauku maradufu kuwa mfalme ayatendee kazi maagizo ya Papa. Baada ya kushindwa na ung’ng’anizi wa balozi huyo wa Papa, alimruhusu kulipeleka shauri lakini mbele ya mkutano. Kwa sababu ya mashaka wale waliompendelea Mwanamatengenezo walikuwa wanaingojea hotuba ya Aleander. Mjumbe wa baraza la uchaguzi wa Saksoni hakuwepo, lakini baadhi ya washauri wake waliiandika hotuba ya balozi huyo wa Papa.TK 95.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents