Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mambo Yanayotukumbusha Kusulubishwa kwa Mwokozi

    Jambo moja linalotukumbusha kusulubishwa litabakia: Mkombozi wetu daima atakuwa na alama za kusulubiwa kwake. Alama pekee za kazi ya ukatili iliyosababishwa na dhambi. Katika kipindi chote cha milele majeraha aliyoyapata Kalvari yataonesha sifa zake na kutangaza uwezo wake.TK 403.3

    Kristo aliwahakikishia wanafunzi wake kwamba alikwenda kuwaandalia makao kwenye nyumba ya Baba yake. Lugha ya binadamu haitoshelezi kuelezea ujira wa wenye haki. Utajulikana tu kwa wale watakaouona. Hakuna akili ya mwanadamu yeyote inayoweza kufahamu utukufu wa Paradiso ya Mungu.TK 403.4

    Katika Biblia urithi wa waliokombolewa unaitwa “nchi” Waebrania 11 : 14-16. Hapo Mchungaji wa mbinguni atawaongoza kondoo wake kwenye vijito vya maji ya uzima. Pale kuna vijito vinavyotiririka vilivyo angavu kama bilauri, na pembeni mwa vijito hivyo miti itakuwa inapepea na kutupa vivuli vyao kwenye njia zilizoandaliwa kwa ajili ya waliokombolewa na Bwana. Tambarare kubwa zinainuka na kuwa vilima vizuri, na vilele vya milima ya Mungu inasimama kwa fahari. Kwenye tambarare zile zilizokuwa zimetulia, kando ya vijito vya uzima, watu wa Mungu, ambao kwa muda mrefu hawakuwa na makao wenye kutangatanga watapata mahali pa kuishi.TK 403.5

    “Nao watajenga nyumba, na kukaa ndani yake; watapanda mizabibu, na kula matunda yake.” “Hawatajenga, akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, akala mtu mwingine: . . . “wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao” . .. Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi.” “Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana- mbuzi; . . na mtoto mdogo atawaongoza.”. .Hawatadhuru wala hawataharibu katika mlima wangu wote mtakatifu; Isaya 65:21,22; 35:1; 11:6,9.TK 403.6

    Maumivu hayawezi kuwepo mbinguni. Hakutakuwa tena na machozi, wala misafara ya mazishi “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, . . .kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.” “Wala hapana mwenyeji atakayesema, Mimi mgonjwa; watu wakaao humo watasamehewa uovu wao.” Ufunuo 21:4; Isaya 33:24.TK 404.1

    Kuna Yerusalemu Mpya, makao makuu ya dunia mpya na yenye utukufu. “Mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri.” “Na mataifa ya waliokombolewa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.” “Maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.” Ufunuo 21:11, 24,3.TK 404.2

    Katika mji wa Mungu “hapatakuwa na usiku” Ufunuo 22:5. Hapatakuwa na kuchoka. Daima tutajisikia kuwa na nguvu ya asubuhi na kuendelea kuwa katika hali hiyo. Mwanga wa jua utazidiwa na mng’ao usiopungua, ambayo unapita mng’ao wa mwezi. Waliokombolewa watatembea katika utukufii wa siku isiyo kuwa na ukomo.TK 404.3

    “Nami sikuona hekalu ndani yake; kwa maana Bwana Mungu Mwenyezi na Mwana-Kondoo, ndio hekalu lake.” Ufunuo 21:22. Watu wa Mungu wanapata fursa ya kuwa na mazungumzo ya wazi na Baba na Mwana. Sasa tunaitazama sura ya Mungu kama vile kwenye kioo, lakini tutakapomwona uso kwa uso, bila kuwa na utaji katikati.TK 404.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents