Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kushinda Kwa Upendo Wa Mungu

  Kule upendo na huruma ambazo Mungu mwenyewe ameweka kwenye mioyo vitapata uzoefu mtamu na wa kweli. Usharika halisi pamoja na viumbe watakatifu na waaminifu wa zama zote uhusiano mtakatifu unaowaweka pamoja. “ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa.” (Waefeso 3:15) -hawa wanasaidia kuleta furaha ya waliokombolewa.TK 404.5

  Pale akili zisizoflkwa na mauti zitaelewa furaha isiyoshindwa ya maajabu ya nguvu ya uumbaji, siri ya upendo wa ukombozi. Kila sehemu itaendelezwa, kila uwezo kuongezeka. Kupatikana kwa maarifa hakutachosha nguvu. Biashara kubwa zinaweza kufanyika, matarajio makubwa yanaweza kufikiwa, na shauku kubwa zinaweza kufikiwa. Na bado kutainuka viwango vya juu kufikia, maajabu mapya ya kustaajabia, kweli mpya za kuelewa, vitu vipya vya kuonesha uwezo wa akili, mwili na roho.TK 405.1

  Hazina zote za ulimwengu zitafunguliwa kwa waliokobolewa na Mungu. Hawatatawaliwa na kifo. Wataaruka pasipo kuchoka kwenda ulimwengu wa mbali. Watoto wa dunia wataingia katika furaha na hekima ya viumbe wasioanguka na watashiriki hazina za maarifa walizozipata vizazi na vizazi. Kwa kuona bila kukoma wanashangaa utukufu wa uumbaji-jua na nyota na mifumo, yote katika utaratibu uliopangwa vikizunguka kiti cha enzi cha Mungu.TK 405.2

  Na miaka ya milele inapoendelea, italeta ufunuo wa utukufu zaidi wa Mungu na Wakristo. Kwa kadri watu watakapojifunza zaidi kuhusu Mungu ndivyo watakavyozidi kuishangaa tabia yake. Wakati Yesu atakapofungua mbele yao utajiri wa ukombozi wao na mafanikio ya kushangaza katika pambano kuu dhidi ya Shetani, mioyo ya waliokombolewa itasisimuka kwa kujitoa, na elfu kumi mara elfu kumi sauti zinainua kiitikio cha sifa.TK 405.3

  “Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na juu ya nchi na chini ya nchi ya juu ya bahari, na vitu vyote vilivyomo ndani yake, nalivisikia, vikisema, Baraka na heshima na utukufu na uweza una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwana-Kondoo, hata milele na milele.” Ufunuo 5:13 Pambano kuu limekwisha. Dhambi na wenye dhambi hawapo tena. Ulimwengu wote ni safi. Pigo moja la usawa na furaha linasambaa katika uumbaji wote. Kuoka kwake yeye aliyeumba vyote, unatiririka uzima na mwanga katika ulimwengu usio na kikomo. Kuanzia kwenye chembe ndogo hadi kwenye ulimwengu mkubwa, vitu vyote vyenye uhai na visivyo na uhai katika uzuri wake halisi vinatangaza Mungu ni upendo.TK 406.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents