Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kutoroka Augsburg

  Marafiki wa Luther walipendekeza kwamba kwa sababu hapakuwa na umuhimu kwake kubaki pale; angepaswa kurejea Wittenberg bila kuchelewa, na pia tahadhari kubwa zichukuliwe. Naye aliufuata mpango huo, akaondoka kwa farasi huko Augsburg kabla ya mapambazuko, akiongozana na mlinzi aliyetolewa na hakimu. Kwa siri alipenya kwenye mitaa ya mji wenye giza. Adui, wakiwa makini na katili, walikuwa wanapanga maangamizi yake. Huo ulikuwa ni wakati wa dukuduku na maombi ya dhati. Akalifikia lango dogo kwenye ukuta wa mji. Lilifunguliwa kwa ajili yake, na akapita akiwa na mlinzi wake. Kabla balozi wa Papa hajagundua kuwa Luther ameondoka, alikuwa ameflka mbali kusikoweza kufikiwa na watesi wake.TK 89.4

  Balozi alipopata taarifa kuwa Luther ametoroka, alishindwa kabisa kwa mshangao na hasira. Alitarajia kupata heshima kubwa sana kwa ujasiri wake katika kumshughulikia huyu mtaabishaji wa kanisa. Katika barua aliyoandika kwa Frederick, mjumbe wa baraza la uchaguzi la Saksoni, balozi alimkosoa Luther vikali, akamtaka Frederick ampeleke Roma au yeye apigwe marufuku huko Saksoni.TK 90.1

  Mjumbe wa baraza la uchaguzi, alifahamu kidogo tu juu ya mafundisho yaliyofanyiwa marekebisho, lakini alivutwa sana na nguvu na usahihi wa maneno ya Luther. Frederick aliazimu kumlinda Luther hadi itakapothibitika kuwa alikuwa na makosa. Katika jibu lake kwa balozi wa Papa Frederick, aliandika: “Kwa sababu Daktari Luther alikuja mbele zako pale Augsburg, ilikupasa uridhike. Hatukutegemea kwamba ungejitahidi kumfanya afute mafundisho yake bila kumwonesha makosa yake. Hakuna mtu miongoni mwa wasomi ndani ya nchi yetu aliyenipa taarifa kuwa mafundisho ya Martin hayamheshimu Mungu, yanampinga Kristo, au ni ya uasi.” 54D’Aubigne, bk. 4, ch. 10. Mjumbe wa baraza Ia kura alitambua kuwa matengenezo yalihitajika. Kwa siri, alifurahi kwamba hisia za mvuto mzuri zilianza kujitokeza kanisani.TK 90.2

  Ni mwaka mmoja pekee ulikuwa umepita tangu Mwanamatengenezo alipobandika Maandiko yake kwenye mlango wa kanisa; lakini maandishi yake yalikuwa yamewasha shauku mpya juu ya Maandiko Matakatifu kila mahali. Wanafunzi walimiminika kwenye Chuo kikuu, siyo kutoka sehemu zote za Ujerumani pekee, lakini kutoka nchi nyingine. Vijana walipouona mji la Wittenberg kwa mara ya kwanza “waliinua mikono yao mbinguni, na kumsifu Mungu kwa kusababisha nuru kutoka mbinguni kuangaza kote kupitia mji huu.” 55Ib d.TK 90.3

  Hadi hapo Luther alikuwa amegeuka kwa sehemu kutoka kwenye makosa ya Kanisa la Roma. Lakini, aliandika, “Ninazisoma amri za Mapapa, na...sifahamu endapo Papa ndiye mpinga Kristo mwenyewe, au mtume wake, kwa hiyo Kristo amepotoshwa na kusulubishwa ndani yao. 56Ibid., bk. 5, ch. 1TK 90.4

  Kanisa la Roma zaidi na zaidi lilikasirishwa na mashambulizi ya Luther. Wapinzani wenye msimamo mkali, hata madaktari kwenye vyuo vikuu vya Wakatoliki, walitangaza kuwa yeye atakayemwua mtawa (Luther) atakuwa hana dhambi. Lakini Mungu alikuwa mlinzi wake. Mafundisho yake yalikuwa yanasikika kila mahali-“katika nyumba za watu na nyumba za watawa...katika majumba ya waheshimiwa, katika vyuo vikuu, na katika makao ya wafalme.” 57Ibid., bk. 6, ch. 2.TK 91.1

  Wakati huu Luther aligundua kuwa ukweli mkuu wa kuhesabiwa haki kwa imani ulikuwa unashikwa na Mwanamatengenezo wa Bohemia, Huss. “Sisi wote” alisema Luther, “Paulo, Augustino, na mimi mwenyewe, tulikuwa wafuasi wa Huss bila kufahamu!” 58Wylic, bk. 6, ch. 1.TK 91.2

  Hivyo Luther aliandika kuhusu vyuo vikuu: “Nina hofu kubwa kwamba vyuo vikuu vitathibitika kuwa malango makuu ya kuzimu, isipokuwa kama watafanya bidii kuyafafanua Maandiko Matakatifu, na kuyaandika ndani ya mioyo ya vijana...kila taasisi ambayo ndani yake watu hawajajazwa na Neno la Mungu daima lazima itaharibika.” 59D’Aubigne, bk. 6, ch. 3.TK 91.3

  Mwito huu ulisambazwa katika Ujerumani yote. Taifa zima lilitikiswa. Wapinzani wa Luther walimtaka Papa achukue hatua za uamuzi dhidi yake. Ilitolewa amri kwamba mafundisho yake yashutumiwe haraka. Mwanamatengenezo na wafuasi wake, kama hawangefuta mafundisho yao, wote wangetengwa.TK 91.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents