Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Imani Inayostahimili

    Wakati wa mateso na maumivu makali ulio mbele yetu utahitaji imani inayoweza kustahimili uchovu, kuchelewa, na njaa, imani ambayo haitazimia hata kama itajaribiwa vikali. Ushindi wa Yakobo ni ushahidi wa nguvu ya maombi yasiyokoma. Wale wote watakaozishikilia ahadi za Mungu kama alivyofanya Yakobo, watashinda kama alivyoshinda. Kupigana mieleka na Mungu-ni wachache kiasi gani wale wanaojua maana yake! Wakati mawimbi ya mashaka yanapomwathiri muombaji, ni wachache sana wanaoshikilia kwa imani ahadi za Mungu.TK 374.1

    Wale ambao wanaonesha imani kidogo sasa, wako katika hatari kuu ya kuangukia kwenye uwezo wa Shetani wa udanganyifu. Na hata kama watastahimili jaribio watatumbukizwa katika mateso mazito wakati wa taabu, hii ni kwa sababu hawakuifanya kuwa tabia yao kumtumainia Mungu. Yatupasa wakati huu tuthibitishe ahadi zake.TK 374.2

    Mara nyingi taabu inakuwa kubwa wakati inapotarajiwa kuliko katika uhalisia, lakini hili sio kweli kuhusiana na Zahama iliyo mbele yetu. Maelezo yaliyo wazi kabisa hayawezi kufikia ukubwa wa majaribu. Wakati huo wa mateso kila nafsi lazima ijisimamie mbele za Mungu.TK 374.3

    Wakati huu ambapo kuhani mkuu anafanya upatanisho kwa ajili yetu, yatupasa tujitahidi kuwa wakamilifu katika Kristo. Mwokozi wetu hakufikishwa hatua ya kuanguka katika jaribu hata kwa wazo moja. Shetani anatafuta mahali ndani ya moyo wa mwanadamu anapoweza kuweka makao, tamaa fulani mbaya inatunzwa, ambayo anaitumia majaribu yake yanapata uwezo wake. Lakini Kristo alisema kuhusu yeye mwenyewe: “Mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.” Yohana 14:30. Shetani hakukupata kasoro yoyote katika maisha ya Mwana wa Mungu ambayo ingemwezesha kupata ushindi. Hakukuwa na dhambi katika maisha yake ambayo Shetani angeitumia kwa manufaa yake. Hii ndio hali wanayotakiwa kuwa nayo wale watakaoshinda katika wakati wa taabu.TK 374.4

    Ni katika maisha haya ndipo tunatakiwa kujitenga na dhambi, kwa njia ya imani katika damu ya upatanisho ya Kristo. Mwokozi wetu wa thamani, anatualika tujiunge naye, tuunganishe udhaifu wetu na nguvu zake, tuunganishe kutostahili kwetu na kufaa kwake. Ni jukumu letu kushirikiana na mbingu katika kazi ya kutengeneza tabia zetu ili zifikie mfano wa mbinguni.TK 375.1

    Kazi ya Shetani ya udanganyifu na uharibifu itafikia katika kilele chake wakati wa taabu. Mionekano ya kutisha ya kiumbe asiye wa kawaida itafunuliwa angani, katika sura ya uwezo wa maShetani wa kutenda miujiza. Roho za maShetani zitaenda kwa “wafalme wa dunia” na duniani kote kuwashawishi ili waungane na Shetani katika jitihada zake za mwisho dhidi ya serikali ya mbinguni. Watu watainuka wakijifanya kuwa wao ni Kristo mwenyewe. Watafanya miujiza ya uponyaji na kukiri kwamba wana ufunuo kutoka mbinguni unaopingana na Maandiko.TK 375.2

    Kama tendo la mwisho katika igizo kuu la udanganyifu, Shetani mwenyewe atamwigiza Kristo. Kanisa kwa muda mrefu limetazamia kuja kwa Mwokozi kama utimilifu wa matumaini yote. Sasa mdanganyifu mkuu atafanya ionekane kuWakristo amekuja. Shetani atajidhihirisha mwenyewe kama kiumbe mwenye nguvu aliye na nuru inayong’ara , akifanana na maelezo ya Mwana wa Mungu katika Ufunuo.(Ufunuo 1:13-15).TK 375.3

    Utukufu utakaomzunguka Shetani haupitwi na kitu chochote ambacho macho ya mwanadamu yamewahi kukiona. Sauti kuu ya ushindi itasikika “Kristo amekuja!” Watu wataanguka kifudifudi mbele zake. Naye atainua mikono yake na kuwabariki. Sauti yake ni laini lakini tamu. Kwa kutumia sauti ya huruma ataeleza baadhi ya kweli zile zile za mbinguni ambazo Mwokozi alizitamka. Ataponya magonjwa, kisha kwa kujifanya ana tabia ya Kristo, atadai kwamba aliibadilisha Sabato kuwa Jumapili. Atasema kwamba wale wanaoishika siku ya saba takatifu wanalikufuru jina lake. Huu ni udanganyifu mkubwa unaoangusha. Wengi watausikiliza uchawi huu, wakisema, “Huu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu.” Matendo 8:10.TK 375.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents