Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Matengenezo Nchini Denmark

  Katika nchi za upande wa Kaskazini Injili iliingia kwa amani. Walipokuwa wanarudi nyumbani kutoka chuoni, wanafunzi wa Wittemberg walikuja nchini Skandinavia na imani ya matengenezo. Maandiko ya Luther yalikuwa yanasambaza nuru pia. Watu shupavu wa upande wa kaskazini waliachana na ufisadi na imani za kishirikina za Kanisa la Roma na kuukaribisha ukweli wa Biblia utoao uzima.TK 155.3

  “Mwanamatengenezo wa Denmark” aliyekuwa anaitwa Tausen, akiwa bado mvulana, alionesha uhodari mkubwa kiakili kwa kujiunga kwenye makazi ya watawa. Mtihani ulidhihirisha kwamba alikuwa na karama zilizo matumaini mema katika utumishi wa kanisa. Kijana huyo aliruhusiwa kuchagua Chuo cha kujiunga nacho kilichoko Ujerumani au Uholanzi, lakini kwa sharti moja: hakutakiwa kwenda Wittemberg kwenye uwezekano wa hatari ya uasi. Ndivyo watawa walivyosema.TK 155.4

  Tausen alikwenda Cologne, mji ulio moja ya ngome za Kanisa la Roma. Kukaa hapa kwa muda mfupi alikuwa amechafuliwa moyo. Na kwa wakati huohuo alisoma Maandiko ya Luther kwa furaha na alikuwa na shauku kubwa kupata mafundisho binafsi ya Mwanamatengenezo huyu. Kwa kufanya hivyo alikuwa anahatarisha msaada kutoka kwa wakuu wake. Baada ya muda mfupi sana alifanya maamuzi na kuwa mwanafunzi wa Wittemberg.TK 156.1

  Aliporudi kwao Denmark hakuifunua siri yake, lakini alidiriki kuwaongoza marafiki zake kwenye imani safi. Alikuwa anaifungua Biblia na kuwafundisha habari za Kristo tumaini la pekee la wokovu kwa mwenye dhambi. Mkuu wa nyumba ya watawa alighadhabika maana alikuwa ameweka tumaini kwake kwamba atakuwa mtetezi wa Kanisa la Roma. Mara moja aliondolewa katika nyumba yake ya kitawa na kuwekwa kizuizini chumbani kwake.TK 156.2

  Kutoka katika vizuizi vya chumba chake Tausen alikuwa anawasiliana na rafiki zake kuhusu elimu ya ukweli. Endapo mapadre hawa wa Denmark wangekuwa na uelewa wa mpango wa kanisa wa kushughulikia “uasi wa kidini”, sauti ya Tausen isingesikika tena, kwa hiyo badala ya kumfungia katika magereza ya chini ya ardhi, walimfukuza toka katika makao ya watawa.TK 156.3

  Amri ya mfalme iliyokuwa imetolewa muda mfupi uliokuwa umepita, ilitoa ulinzi kwa walimu waliokuwa wanafundisha mafundisho mapya. Makanisa yalikuwa yanamkaribisha, na watu walikuwa wanafurika kuja kumsikiliza. Agano Jipya kwa lugha ya watu wa Denmark lilikuwa linasambazwa kwenye maeneo mengi. Juhudi za kutaka kuiangusha kazi hiyo zilisaidia tu kuieneza, na kwa muda mfupi Denmark ilitangaza kuipokea imani ya matengenezo.TK 156.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents