Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Fumbo la Patakatifu Lafumbuliwa

    “Hema ya kweli” iliyo mbinguni ndiyo patakatifii pa agano jipya. Wakati Kristo alipokufa huduma kielelezo zilikoma. Kwa kuwa Danieli 8:14 ilitimia katika kipindi cha agano jipya, basi patakatifu panapozungumziwa hapa ni lazima pawe pa agano jipya. Kwa hiyo unabii unaosema “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa,” unahusu patakatifu pa mbinguni.TK 260.3

    Lakini kutakaswa kwa patakatifu ni nini? Je, kunaweza kukawa na kitu cho chote cha kutakaswa mbinguni? Katika Waebrania 9 kutakaswa kwa patakatifu pa duniani na patakatifu pa mbinguni panaelezewa: “Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo. Basi ilikuwa sharti nakala za mambo yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasaflshwe kwa dhabihu zilizo bora kuliko hizo” (Waebrania 9:22, 23), yaani damu ya Kristo iliyo na thamani.TK 260.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents