Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 35 - Kutishiwa Kwa Uhuru Wa Dhamiri

  Waprotestanti sasa, wanaujali Ukatoliki zaidi ya ilivyokuwa katika miaka iliyotangulia. Katika zile nchi ambazo Ukatoliki unachukua hatua za mapatano ili kupata ushawishi, kuna mtazamo unaopata nguvu kwamba, hatutofautiani sana kwenye mambo ya msingi kama ilivyokuwa inadhaniwa na kwamba maafikiano kidogo kwa upande wetu yatatuleta kwenye maelewano mazuri zaidi na Kanisa la Roma. Ulikuwepo wakati ambapo Waprotestanti waliwafundisha watoto wao kuwa kutafuta mapatano na Kanisa la Roma itakuwa ni kukosa uaminifu kwa Mungu. Lakini sasa tofauti ya mawazo yanayotolewa ni kubwa!TK 343.1

  Watetezi wa utawala wa Papa wanatamka kuwa kanisa limekashifiwa, kwamba si halali kulihukumu kanisa la sasa kwa utawala wake wa kame za ujinga na giza. Wanautolea udhum ukatili wake wa kutisha kuwa ulikuwa ni ushenzi wa nyakati hizo.TK 343.2

  Je, watu hawa wameyasahau madai yanayotolewa na utawala huu kwamba kanisa halikosei? Kanisa la Roma linadai kuwa, “Kanisa halikukosea; na wala, kulingana na Maandiko halitakosea” 235 ohn L. von Mosheim, Institute of Ecclesiastical History, book 3, century 11, part 2, chapter 2, section 9, note 17.TK 343.3

  Kanisa la Papa halitayaacha madai yake ya kutokosea. Hebu vikwazo vinavyowekwa na serikali za mataifa viondolewe na Kanisa la Roma limdishwe kwenye utawala wake wa zamani, kutakuwa na uamsho wa udhalimu wake na mateso.TK 343.4

  Ni kweli kwamba kuna Wakristo wazuri ndani ya ushirika wa Kanisa Katoliki la Roma. Maelfu ya watu katika kanisa lile wanamtumikia Mungu kwa uaminifu kulingana na num waliyonayo. Mungu anawaangalia kwa humma na upole watu hawa ambao, wameelimishwa katika imani yenye udanganyifu na isiyokidhi haja. Atawaletea num ya ukweli ili ipenye katika giza na wengi watajiunga na watu wa Mungu.TK 343.5

  Lakini Ukatoliki kama mfumo hauna upatanifu na Injili ya Kristo sasa zaidi ya ilivyokuwa katika kipindi chochote cha nyuma. Kanisa la Roma linatumia kila mbinu kupata upya udhibiti wa dunia, kuyaanzisha tena mateso, na kuyaharibu yale yote ambayo Uprotestanti umeyafanya. Ukatoliki unapata nguvu kila upande. Angalia idadi ya makanisa yake inavyoongezeka. Tazama umaarufu wa vyuo na shule zake, Waprotestanti wakiwa wateja wao wakubwa. Angalia ukuaji wa kanuni za ibada huko Uingereza na dosari za mara kwa mara kwenye ngazi za uongozi za Wakatoliki.TK 344.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents