Huss Afa kwa Kuchomwa Moto
Aliongozwa sasa kutoka pale alipokuwa. Msafara mkubwa ulifuata. Wakati kila kitu kilipokuwa tayari kwa ajili ya moto kuwashwa, mfia dini huyu alishawishiwa kujiokoa mwenyewe kwa kukana makosa yake. “Makosa gani,” alihoji Huss, “nikane? Ninajua sina hatia ya hata moja. Ninamuita Mungu kushuhudia kwamba yote niliyoandika na kuhubiri yamekusudiwa kuokoa roho toka dhambini na upotevuni; kwa hiyo, kwa furaha sana nitathibitisha kwa damu yangu ukweli huo ambao nimeuandika na kuuhubiri.” TK 70.2
Wakati miali ya moto ilipowaka kumzunguka, alianza kuimba, “Yesu, wewe Mwana wa Daudi, unirehemu mimi,” na aliendelea hivyo hadi sauti yake iliponyamazishwa milele. Mkereketwa wa mamlaka ya Papa, akielezea ufia dini wa Huss na Jerome, ambaye alikufa muda mfupi tu baadaye, alisema: “Walijiandaa kwa ajili ya moto kana kwamba walikuwa wakienda kwenye sherehe ya harusi. Hawakutoa kilio chochote cha maumivu. Wakati miali ilipopanda, walianza kuimba nyimbo; na ilikuwa shida kwa ukali wa moto kukomesha kuimba kwao.” TK 70.3
Baada ya mwili wa Huss kuteketezwa na moto, majivu yake yalikusanywa na kutupwa kwenye mto Rhine, na hapo yakapelekwa na maji hadi baharini na kuwa mbegu iliyosambazwa kwenye nchi zote za dunia. Katika nchi ambazo hazikufahamika bado, ingezaa matunda kwa wingi kwa njia ya shuhuda za ukweli. Sauti katika ukumbi wa baraza la Constance iliamsha miangwi ambayo imekuwa ikisika katika kame zote zilizofuata. Mfano wake ungewatia moyo watu wengi kuweza kusimama imara wanapokabili mateso na mauti. Kuuawa kwake kulidhihirisha kwa ulimwengu ukatili wa kilaghai wa Kanisa la Roma. Maadui wa ukweli walikuwa wakiiendeleza kazi ambayo walifikiri waniuangamiza!TK 71.1
Bado damu ya shahidi mwingine ilikuwa lazima ishuhudie ukweli. Jerome alikuwa amemtia moyo Huss kuwa na ujasiri na uthabiti, akimwahidi kwamba kama angeingia kwenye hatari, angemkia pale ili kumsaidia. Aliposikia juu ya kufungwa kwa Mwanamatengenezo, mwanafunzi huyu mwaminifu alijiandaa kukamilisha ahadi yake. Bila ya hati ya usalama alielekea Constance. Alipofika, alishawishika kuwa alikuwa amejiweka hatarini mwenyewe bila kuweza kufanya lolote kwa ajili ya Huss. Alianza kukimbia lakini alikamatwa na kuletwa akiwa amefungwa kwenye minyororo. Aliposimama kwa mara ya kwanza mbele za baraza, alipojaribu kujibu alikutana na kelele, “Achomwe naye!” Alitupwa kwenye gereza ardhini ambapo alilishwa mkate na maji. Ukatili wa gerezani ulipelekea kuugua kwake hadi kutishia uhai wake; na maadui zake, wakihofu kwamba angewatoroka, waliTK 71.2