Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jinsi Mafundisho ya Uongo Yalivyoingia

    Hata kabla ya kuanzishwa kwa utawala wa Papa mafundisho ya wanafalsafa wapagani yalikuwa yameshakuwa na ushawishi kanisani. Wengi bado walikuwa wanang’ang’ania itikadi za falsafa ya kipagani na kulazimisha watu wajifunze falsafa hiyo kama njia ya kueneza ushawishi wao miongoni mwa wapagani. Makosa makubwa yaliingizwa katika imani ya Kikristo kwa njia hiyo.TK 40.3

    Katika mafundisho hayo, fundisho lililokuwa maarufu zaidi ni ile imani ya kutokufa kwa mwanadamu na hali ya kuwa na ufahamu akiwa mautini. Fundisho hili liliweka msingi ambapo Kanisa la Roma lilianzisha kuomba kwa watakatifu na kumwabudu bikira Maria. Kutoka katika jambo hilo pia likaibuka fundisho la uongo la mateso ya milele kwa wale ambao hawatatubu, ambalo liliingizwa mapema katika imani ya Papa.TK 40.4

    Njia iliandaliwa kwa ajili ya uzushi mwingine wa upagani - yaani toharani, ambao uliokuwa unatumika kuwatishia watu wengi wenye mapokeo potovu. Fundisho hili la uongo lilikuwa linadai kuwa kuna mahali pa mateso ambapo roho za watu ambao hawajastahili hukumu ya jehanum hupata adhabu kwa ajili ya dhambi zao, na baada ya hapo zikitakasika, huruhusiwa kuingia mbinguni. (Angalia Kiambatisho.)TK 41.1

    Ulikuwa unahitajika uongo mwingine kuliwezesha Kanisa la Roma kunufaika kutokana na hofu na uovu wa wafuasi wake: fundisho la kulipia msamaha. Ahadi ya ondoleo la dhambi, za zamani, za sasa na zijazo ilitolewa kwa wote ambao wangejiandikisha katika vita vya Papa vya kuwaadhibu maadui zake au kuwaangamiza wale waliokuwa wanathubutu kukataa ukuu wake wa kiroho. Kwa kulipa pesa kanisani, watu waliweza kuondokana na dhambi na pia kuzifungulia roho za rafiki zao zilizokuwa zinateseka motoni. Kwa njia hiyo, Kanisa la Roma lilizijaza hazina zake na kuendeleza fahari, anasa, na uovu wa waliokuwa wanajifanya wawakilishi wake Yeye ambaye hakuwa na mahali pa kulaza kichwa chake. (Angalia Kiambatisho).TK 41.2

    Nafasi ya meza ya Bwana ilikuwa imechukuliwa na dhabihu ya ibada ya sanamu, yaani misa. Mapdre wa Kanisa la Roma walikuwa wanajifanya kuwa wanaubadili mkate wa kawaida na divai kuwa “mwili na damu halisi Wakristo.” 3Cardinal Wiseman’s Lectures on “The Real Presence, ” lecture 8, sec. 3, par.26. Kwa ufidhuli wenye kufuru, walidai wazi wazi kuwa wana uwezo wa kumwumba Mungu, ambaye ni Mwumbaji wa vyote. Wakristo walikuwa wanalazimishwa, kukiri imani yao katika fundisho hili potovu linalotukana Mbingu, la sivyo wauawe.TK 41.3

    Katika kame ya kumi na tatu kilianzishwa chambo cha kutisha kabisa katika mamlaka ya Papa. -Mahakama ya kanisa ya kukomesha uasi. Katika mabaraza yao ya siri Shetani na malaika zake walitawala akili za watu waovu. Malaika wa Mungu alisimama kati yao, bila kuonekana, akichukua taarifa za kutisha za uamuzi wao mbovu na kuandika historia ya matendo mabaya yasiyofaa kuonekana katika macho ya wanadamu. “Babeli mkuu” alikuwa “amelewa kwa damu ya watakatifu.” Soma Ufunuo 17:5, 6. Miili iliyokuwa imeharibika, ya mamilioni ya wafia dini ilimlilia Mungu kwa ajili ya kisasi juu ya mamlaka iliyokuwa imeasi.TK 41.4

    Utawala wa Papa ulikuwa umekuwa utawala dhalimu wa dunia. Wafalme walikuwa wanatii maagizo ya Papa. Kwa mamia ya miaka, mafundisho ya Kanisa la Roma yalikuwa yanapokelewa bila maswali. Watumishi wake walikuwa wanaheshimiwa na kutunzwa kwa gharama kubwa. Kanisa la Roma lilikuwa halijawahi kufikia ukuu, fahari, na nguvu, kuliko wakati huo.TK 42.1

    Lakini “mchana wa utawala wa Papa ulikuwa ni usiku wa manane kwa ulimwengu.” 4Wylie, History of Protestantism, book 1, Chap. 4. Maandiko yalikuwa hayajulikani kabisa. Viongozi wa utawala wa Papa walikuwa wanaichukia nuru ambayo ingefichua dhambi zao. Sheria ya Mungu, ambayo ni kiwango cha haki, ikiwa imeondolewa, walifanya uovu bila kizuizi. Majumba ya Mapapa na maaskofu yalikuwa mahali pa ufisadi mbaya wa kupindukia. Baadhi ya maaskofu walikuwa wanafanya uhalifu wa kuudhi mpaka watawala wa kidunia wakadiriki kuwaondoa kama watu katili wasioweza kuvumiliwa. Kwa kame kadhaa, Ulaya haikuwa na maendeleo yo yote katika elimu, sanaa, au ustaarabu. Ukristo ulikuwa umekumbwa na kudumaa kimaadiali na kielimu. Hayo ndiyo yalikuwa matokeo ya kuliondoa Neno la Mungu.TK 42.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents