Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 6 - Mashujaa Wawili Wakabili Mauti

  Karibuni kabisa na kame ya tisa Biblia ilikuwa imetafsiriwa na ibada za hadhara zilikuwa zikiendeshwa katika lugha ya watu wa Bohemia. Lakini Gregory VII alikusudia kuwafanya watu watumwa, na tamko lilitolewa lililokataza ibada za hadhara katika lugha ya Bohemia. Papa alitamka kuwa “ilikuwa inapendeza kwa Yeye aliye na uwezo wote kwamba ibada zake ziadhimishwe katika lugha isiyojulikana.” 14Wylie, bk. 3, ch. 1 Lakini mbingu ilitoa mawakala kwa ajili ya kulilinda kanisa. Wawaldensia na Waalbijensi wengi, wakiwa wamekimbizwa na mateso, walikuja Bohemia. Walifanya kazi kwa juhudi na kwa siri. Kwa njia hiyo, Imani ya kwel ilillindwa.TK 63.1

  Kabla ya siku za Huss walikuwepo watu katika Bohemia waliolaani upotovu kanisani. Hofu ya mamlaka ya Papa iliibuliwa, na mateso yakaanzishwa dhidi ya Injili. Baada ya muda tamko lilitolewa kuwa wale waliotoka katika ibada ya Kanisa la Roma wachomwe moto. Lakini Wakristo walitazamia mbeleni ushindi wa kazi yao. Mmoja wao alisema akikaribia kufa, “Kutokea kati ya watu wa kawaida, atainuka mtu asiye na upanga wala mamlaka, nao hawataweza kumshinda.” 15Ibid Yupo ambaye tayari alikuwa akiinuka, ambaye ushuhuda wake dhidi ya Roma ungeamsha mataifa.TK 63.2

  John Huss alizaliwa katika mazingira ya kimaskini na akawa yatima mapema katika maisha yake kutokana na kifo cha baba yake. Mama yake ambaye alikuwa mcha Mungu, hali akiithamini elimu na uchaji wa Mungu kama hazina ya thamani zaidi, alitafuta njia za kumpa mtoto wake urithi huu. Huss alisomea kwenye shule ya jimbo, na kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Prague, akipokelewa kama mwanafunzi aliyesomeshwa kwa msaada.TK 63.3

  Pale chuoni, Huss alijipatia heshima upesi kwa maendeleo yake ya haraka. Mvuto ulioonekana katika mwenendo wake wa uungwana ulimpa heshima kwa wote. Alikuwa mfuasi wa dhati wa Kanisa la Roma na mhitaji makini wa baraka za kiroho ambazo kanisa lilidai kuwa nazo. Baada ya kumaliza mafunzo yake ya chuo, aliingia kwenye upadre. Huku akiongezeka kwa kasi katika umaarufu, aliambatanishwa na makao ya mfalme. Alifanywa pia kuwa profesa na baadaye akawa mkuu wa Chuo Kikuu. Msomi mnyenyekevu aliyesaidiwa akawa fahari ya nchi yake, jina lake lilifahamika Ulaya kote.TK 64.1

  Jerome, ambaye baadaye alikuja kuwa karibu sana na Huss, alikuwa amemletea maandishi ya Wycliffe kutoka Uingereza. Malkia wa Uingereza, muongofu wa mafundisho ya Wycliffe, alikuwa ni mzaliwa wa Bohemia. Kupitia kwa mvuto wake, kazi za Mwanamatengenezo zilisambazwa sana katika nchi yake ya asili. Huss alikuwa na mwelekeo wa kukubali matengenezo yaliyokuwa yakitetewa. Ingawa hakujua, alikuwa tayari amekwisha ingia katika njia ambayo ilikuwa inampeleke mbali zaidi na Roma.TK 64.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents