Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kuiweka Pembeni Sheria ya Mungu

    Wale wanaowafundisha watu kuzichukulia juu juu sheria za Mungu wanapanda uasi ili wavune uasi. Hebu sheria yote ya Mungu itupiliwe mbali, na sheria ya mwanadamu itapuuzwa. Matokeo ya kupuuzia sheria za Mungu yatakuwa na madhara ambayo hayakutarajiwa. Mali za watu hazitakuwa salama, watu watachukua mali za majirani zao kwa nguvu na wenye nguvu ndio watakao kuwa matajiri. Hata maisha yenyewe hayataheshimiwa, kiapo cha ndoa hakitakuwa tena ngome ya kuilinda familia. Aliye na nguvu anaweza kumchukua mke wa jirani yake kwa nguvu. Amri ya tano na ya nne zitawekwa pembeni. Watoto hawatajizuia kuuondoa uhai wa wazazi wao ikiwa kwa kufanya hivyo watapata kutimiza shauku ya mioyo yao iliyopotoka. Ulimwengu uliostaarabika utageuka kuwa genge la vibaka na wauaji, furaha na amani vitatoweka duniani.TK 354.2

    Tayari fundisho hili limefungulia mafuriko ya upotovu duniani. Rushwa na kukosa uadilifu vinafagia kama wimbi kubwa. Hata katika kaya za Wakristo kuna unafiki, talaka, kusaliti viapo vitakatifu na kuendekeza tamaa. Kanuni za kidini, msingi wa maisha ya jamii inaonekana ni jabali linaloyumbayumba tayari kuanguka. Wahalifu sugu mara nyingi wamekuwa wakipewa heshima kana- kwamba ni watu wa pekee wa kuonewa husuda. Umaarufu mkubwa umewekwa katika makosa yao. Vyombo vya habari vinawaongoza watu katika mambo mabaya, na kuwaongoza wengine katika udanganyifu, uporaji na mauaji. Kushawishi maovu, kutokuwa na kiasi na uasi wa kila namna kutainuka. Je, nini kifanyike ili kujiepusha na wimbi la uovu?TK 354.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents