Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwisho Mbaya wa Waovu

  Tabia ya Shetani haitbadilika. Kwa mara nyingine, Uasi kama mkondo wa maji wenye nguvu unaibuka. Ataazimu kutoacha jitihada zake za mwisho dhidi ya Mfalme wa mbinguni. Lakini sasa, katika mamilioni wasiohesabika aliowashawishi kuasi, hakuna atakayetambua ukuu wake. Waovu watakuwa wamejazwa na chuki ile ile ya Mungu inayomchochea Shetani, lakini wataona kwamba hali yao haina namatumaini. “Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu. basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako. Watakushusha hata shimoni. . . . nami nimekuangamiza, Ewe kerubi ufunikaye, utoke katika mawe hayo ya moto. . . . nimekutupa chini, nimekulaza mbele ya wafalme, wapate kukutazama. . . nami nimekufanya kuwa majivu juu ya nchi, machoni pa watu wote wakutazamao. . .umekuwa kitu cha kutisha, wala hutakuwapo tena hata milele.” Ezekieli 28:6-8,16-19.TK 402.1

  “Maana Bwana ana ghadhabu juu ya mataifa yote” “Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu la kikombe chao.” Isaya34:2; Zaburi 11:6. Moto utashukakutoka mbinguni kwa Mungu. Dunia itavunjika. Miali ya moto ulao unaoteketeza utaibuka kutoka kwenye nyufa ardhini. Miamba yenyewe itashika moto. Vitu vitaunguzwa kwa moto mkali, dunia pia na matendo yaliyomo humo yataunguzwa. 2 Petro3:10. Uso wa dunia unaonekana kama tope kubwa, ziwa kubwa la moto. Ni “siku ya kisasi cha Bwana, mwaka wa malipo, ili kushindania Sayuni.” Isaya 34:8.TK 402.2

  Waovu wanaadhibiwa “sawasawa na matendo yao.” Shetani atateseka sio tu kwa uasi wake lakini kwa dhambi zote alizosababisha watu wa Mungu kutenda. Hatimaye katika moto waovu wataangamizwa, mzizi na tawi-Shetani ndiye mzizi na wafuasi wake ni matawi. Adhabu kamili kwa uasi wa sheria imekwisha kutolewa; hitaji la haki yamekwisha kutimizwa. Kazi ya Shetani ya uharibifu imekomeshwa milele. Sasa viumbe wa Mungu wamekombolewa milele kutoka kwenye majaribu yake.TK 402.3

  Wakati dunia itakupokuwa imefunikwa kwa moto, wenye haki wataendelea kukaa salama katika Mji wa Mtakatifu. Wakati Mungu ni moto ulao kwa waovu, kwa watu wake yeye ni ngao. Angalia Ufunuo 20:6; Zaburi 84:11.TK 403.1

  “Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita.” Ufunuo 21:1. Moto utakaowaangamiza waovu utaitakasa dunia. Kila dalili ya laana itaondolewa. Hakuna moto wa kuzimu unaowaka milele utakaowafanya waliokombolewa kuwa na hofu ya matokeo mabaya ya dhambi.TK 403.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents