Tunda la Mafundisho Mapya Ladhihirika
Watu waliongozwa kuipuuza Biblia au kuitupilia mbali kabisa. Wanafunzi walipiga teke vizuizi vyote, wakaachana na masomo yao na kuondoka katika Chuo Kikuu. Watu waliodhania kuwa walikuwa na uwezo wa kufanya uamsho na kuongoza jukumu la Matengenezo walifanikiwa tu kuyapeleka kwenye ukingo wa uharibifu. Watawala wa Kanisa la Roma walifanikiwa tena kumdisha matumaini yao na walishangilia kwa furaha huku wakitamka: “Bado pambano moja la mwisho, na yote yatakuwa ya kwetu.”TK 121.3
Aliposikia kile kilichotokea akiwa Wartburg, Luther alisema kwa mguso: “Siku zote nategemea Shetani kutuletea pigo hili.” Alitambua tabia halisi ya “manabii hao wa kujifanya.” Upinzani wa Papa na mfalme kwa wakati huu ulisababisha mkanganyiko mkubwa. Kutoka kwa marafiki waliokuwa wamekiri Matengenezo, waliibuka maadui wabaya sana waliokuwa wanachochea machafuko na kuleta mtafaruku.TK 121.4
Luther alikuwa ameongozwa na Roho wa Mungu na alikuwa ametumiwa kuliko uwezo wake ulivyokuwa. Lakini mara kwa mara alitetemeka kwa matokeo ya kazi yake: “Kama ningetambua ya kwamba mafundisho yangu yalikuwa yamemjeruhi mtu mmoja, mtu mmoja tu; hata kama fundisho hilo lilikuwa duni na lisiloeleweka kiasi gani-jambo ambalo haliwezekani kwa sababu ni Injili yenyewe-ingekuwa heri nife mara kumi kuliko kuifuta kauli hiyo.” Jiji la Wittenberg lenyewe lilikuwa limeangukia mikononi mwa watu wenye itikadi kali ya kidini na vitendo vya kihalifu vilivyokithiri. Katika nchi yote ya Ujerumani, adui wote waliona kuwa Luther alihusika kwa vitendo hivyo. Kwa uchungu wa moyo Luther aliuliza, “Je, huo ndiyo unaweza kuwa mwisho wa kazi hii kubwa ya Matengenezo?” Alipokuwa akijibidisha kumwomba Mungu amani ilijaa na kufurika moyoni mwake. Alisema, “Kazi hii si yangu bali ni Yako.” Aliazimia kurudi Wittenberg.TK 122.1
Alikuwa chini ya marufuku ya himaya ya Kanisa la Roma. Adui zake walikuwa na uhuru wa kuamua kuutoa uhai wake, marafiki walikuwa wamezuiwa kumpatia hifadhi. Lakini aliona kazi ya Injili ilikuwa hatarini, na kwa jina la Bwana aliondoka pasipo hofu yoyote kwenda vitani kwa ajili ya ukweli. Katika waraka aliomwandikia mbunge, Luther alisema, “Ninakwenda Wittenberg chini ya ulinzi wa juu kuliko ule wa wakuu na wabunge. Sihitaji kuomba msaada wako mheshimiwa, na sihitaji kabisa ulinzi wako, ingependeza zaidi kama mimi ningekulinda wewe.”TK 122.2
Hakuna upanga wowote unaoweza kuendeleza kazi hii. Mungu pekee ndiye atakayefanya mambo yote.” Katika waraka wake wa pili Luther aliongeza maneno haya: “Niko tayari kukukasirisha mheshimiwa na kuchukiwa na ulimwengu wote. Je, watu wa Wittenberg siyo kondoo wangu? Je, hainipasi, ikilazimu; kujitoa kufa kwa ajili yao?” TK 122.3