Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hatia ya Dhambi

  Hatua ya kwanza ya upatanisho na Mungu ni kugundua hatia ya dhambi. “Dhambi ni uasi wa sheria” “kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria.” lYohana3:4. Warumi 3:20. Ili kugundua hatia, mwenye dhambi ni lazima aijaribu tabia yake kwa kutumia kioo cha Mungu kinachoonesha ukamilifu wa tabia ya haki na kumwezesha kuyaona mapungufu yake mwenyewe.TK 289.2

  Sheria humfunulia mwanadamu dhambi yake lakini haitoi suluhisho. Inatangaza kuwa mauti ni fungu la mwenye dhambi. Ni Injili ya Kristo pekee iwezayo kumweka huru dhidi ya hukumu au unajisi wa dhambi. Ni lazima afanye toba kwa Mungu, ambaye sheria yake imevunjwa, na amwamini Yesu ambaye ndiye kafara yake ya upatanisho. Ndipo atapata, “kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilizotangulia kufanywa.” Warumi 3:25. Na anakuwa mtoto wa Mungu.TK 289.3

  Je, sasa yupo huru kuivunja sheria ya Mungu? Paulo anasema: “Basi, je! twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.” “Hasha! Sisi tulioifla dhambi tutaishije tena katika dhambi?” Yohana anatamka kwamba: “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.” Katika kuzaliwa upya, moyo unaletwa kwenye upatanifu na Mungu, kwenye muafaka na sheria yake. Badiliko hili likitokea ndani ya mwenye dhambi, anakuwa ametoka kwenye mauti na kwenda kwenye uzima, kutoka kwenye dhambi na uasi kwenda kwenye utii na uaminifu. Maisha ya zamani yamekoma; maisha mapya ya upatanisho, imani,na upendo yameanza. Ndipo, “maagizo ya torati” yatatimizwa ndani yetu sisi, tunaoenenda sio kwa kuufuata mwili, bali roho. Lugha ya moyo itakuwa: “Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.” Warumi 3:31; Warumi 6:2; lYohana 5:3; Warumi 8:4; Zaburi 119:97.TK 289.4

  Pasipo sheria wanadamu hawawezi kuwa na hatia ya kweli ya dhambi na hawatahitaji toba. Hawatambui hitaji lao la damu ya Kristo inayofanya upatanisho. Tumaini la wokovu limekubaliwa pasipo badiliko la dhati la moyo ama matengenezo ya maisha. Hivyo kuna uongofu wa juu juu na idadi ni kubwa, watu wengi wanaojiunga na kanisa ambao bado hawajajiunga na Kristo..TK 290.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents