Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 42 - Amani Ya Milele: Pambano Lafika Mwisho

  Mwisho wa miaka 1,000 Kristo atarudi duniani akisindikizwa na waliokombolewa na jeshi la malaika. Atawaamuru waovu walikufa kufufuka ili wapokee hukumu yao. Watafufuka, watakuwa hawahesabiki kama mchanga wa bahari, wakiwa na dalili za ugonjwa na mauti. Tofauti iliyoje baina ya wale waliofufuliwa kwenye ufufuo wa kwanza!TK 396.1

  Kila jicho litakuwa limegeuka kuutazama utukufu wa Mwana wa Mungu. Kwa sauti moja jeshi la waovu litasema: “Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana” Mathayo 23:39. Si upendo utakaosababisha tamko hili. Nguvu ya ukweli italazimisha maneno kutoka kwenye midomo isiyoradhi kutamka. Kama ilivyokuwa wakati walipolala katika makaburi yao, waovu watafufuka wakiwa na uadui ule ule kwa Kristo, wakiwa na roho ile ile ya uasi. Hawatapata kipindi kingine cha rehema ili kurekebisha maisha yao yaliyopita.TK 396.2

  Nabii anasema: “Miguu yake itasimama juu ya mlima wa Mizeituni, . . . nao mlima wa Mizeituni utapasuka katikati yake.”Zekaria 14:4. Yerusalemu Mpya utakaposhuka kutoka mbinguni, utakaa juu ya mahali palipotayarisha, na Kristo na watu wake na malaika wataingia kwenye mji mtakatifu.TK 396.3

  Akiwa amekatiliwa mbali na kazi zake za udanganyifu, mkuu wa uovu atakuwa na huzuni na kuvunjika matumaini, lakini waovu waliokufa watakapofufuliwa na atakapouona mkutano mkubwa ukiwa upande wake, matumaini yake yatakuwa hai. Hakusudii kushindwa katika pambano kuu. Atawapanga waliopotea chini ya bendera yake. Kwa kumkataa Kristo waliukubali utawala wa mwasi, walikuwa tayari kutimiza amri zake. Akiwa bado na hila zake za awali, atakataa kukiri kuwa yeye ni Shetani. Atadai kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa dunia ambaye urithi wake ulinyanganywa pasipo uhalali. Atajionesha mwenyewe kuwa ni mkombozi, akiwahakikishia wale aliowadanganya kuwa ni uwezo wake uliowafufua kutoka makaburini mwao. Shetani atawafanya walio dhaifu kuwa na nguvu, na atawavuvia wote kwa uwezo wake kuwaongoza kuutwaa mji wa Mungu. Anawaonesha mamilioni wasiohesabika waliofufuliwa kutoka katika wafu, na atatamka kuwa yeye kama kiongozi wao anaweza kutawala katika enzi na ufalme wake.TK 396.4

  Kwenye mkutano huu mkubwa kutakuwa na jamii ya watu walioishi muda mrefu waliokuwepo kabla ya gharika, watu wa kimo kirefu na uwezo mkubwa wa akili; watu ambao matendo yao ya ajabu yaliifanya dunia kuabudu akili zao, lakini ni watu ambao ukatili na mavumbuzi yao maovu yalisababisha Mungu awafute kwenye uumbaji wake. Watakuwepo wafalme na majenerali ambao hawakuwahi kushindwa katika pambano hata moja. Walipokuwa wamekufa hawakupitia mabadiliko yoyote. Watakapotoka makaburini watahamasishwa na nia ileile ya kushinda iliyowatawala wakati walipoanguka.TK 397.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents