Maendeleo Nchini Sweden
Kule Sweden pia, vijana kutoka Wittemberg walikwenda na maji ya uzima kwa watu wa nchi yao. Viongozi wawili wa Matengenezo wa Sweden, Olaf na Laurentius Petri, walikuwa wamejifunza chini ya Luther na Melanchthon. Kama alivyokuwa Mwanamatengenezo mkuu, Olaf alikuwa akiwagusa watu kwa ustadi wake wa kuzungumza, wakati Laurentius, kama alivyokuwa Melanchthon, alikuwa ni mtu mtulivu na mwangalifu sana. Wote walikuwa thabiti na wasioogopa. Mapadre wa Kanisa Katoliki waliwachochea watu waliokuwa hawajui chochote na wenye imani za kishirikina. Mara kadhaa Olaf Petri aliponea chupuchupu kuuawa. Hata hivyo Wanamatengenezo hawa walikuwa wanalindwa na mfalme ambaye alikuwa amedhamiria imani ya matengenezo iendelee na alikuwa amewakaribisha wasaidizi hawa wenye uwezo kwenye pambano dhidi ya Kanisa la Roma.TK 156.5
Mbele ya mfalme na viongozi mbalimbali wa nchi ya Sweden, kwa uwezo mkubwa Olaf Petri aliitetea imani ya matengenezo. Alisema kwamba mafundisho ya mababu yapokelewe tu iwapo yatakubaliana na Maandiko; na kwamba mafundisho ya misingi ya imani yametolewa kwenye Biblia kwa njia dhahiri, ili watu wote waelewe. Shindano hili linatumika kutuonesha kuwa “watu waliokuwa wa kawaida ndiyo waliokuwa wameunda jeshi la Wanamatengenezo. Hawakuwa watu wasiojua kusoma na kuandika, ama wafuasi wa vikundi mbalimbali vya kidini au wabishani wenye makelele-hawakuwa watu wa aina hiyo. Walikuwa watu waliosoma Neno la Mungu na kujua vyema kuzitumia silaha walizokuwa wamepewa na Biblia. Walikuwa wasomi na wanateolojia, watu waliokuwa wameutawala mfumo wote wa ukweli wa Injili, ambao walishinda kwa urahisi dhidi ya wapotoshaji wa mafundisho na wakuu wa Kanisa la Roma.” TK 157.1
Mfalme wa Sweden aliipokea imani ya Kiprotestanti, na bunge la nchi hiyo liliunga mkono hoja hiyo. Kwa kibali cha mfalme ndugu hao wawili waliitafsiri Biblia yote. Ilikuwa imeamriwa kwenye mkutano wa kidini kuwa katika ufalme wote wachungaji wafundishe Maandiko na watoto wafundishwe kusoma Biblia shuleni.TK 157.2
Kukombolewa kwa taifa hili kutoka kwenye ukandamizaji wa Kanisa la Roma, kulilifanya kufikia ukuu na uthabiti ambao ulikuwa haujafikiwa hapo kabla. Kame moja baadaye, taifa hili lililokuwa dhaifu-taifa pekee katika Ulaya yote liliisaidia Ujerumani kujikomboa toka kwenye pambano la kuogofya la Vita vya Miaka Thelathini. Ulaya ya Kaskazini yote ilikuwa inaonekana kumdishwa tena kwenye utawala wa kidikteta wa Kanisa la Roma. Majeshi ya Sweden yaliiwezesha Ujerumani kupata ushindi wa kuvumiliwa kwa Waprotestanti na kurejesha uhuru wa dhamiri katika nchi zilizokuwa zimepokea imani ya Matengenezo.TK 158.1