Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Maandiko na Matukio ya Miaka

  Maandiko haya na mengine yalimthibitishia Miller kwa uwazi kuwa utawala wa amani kwa ulimwengu mzima na kusimamishwa kwa ufalme wa Mungu duniani kutakuwa baada ya kuja kwa Yesu mara ya pili. Zaidi ya hayo aliona kuwa hali ya ulimwengu ililingana na maelezo ya unabii wa siku za mwisho. Alilazimika kufikia hitimisho kuwa muda ambao dunia ilipewa katika hali yake ya sasa ulikuwa karibu kutimia.TK 208.1

  “Ushahidi mwingine ambao ulikuwa na mguso hai katika moyo wangu” Miller alisema, “ni mtiririko wa matukio katika Maandiko Niligundua kuwa matukio yaliyotabiriwa ambayo yalitimizwa wakati uliopita, mara zote yaliyotokea ndani ya wakati uliowekwa matukio kwanza yalikuwa ni jambo la unabii tu, yalitimizwa kulingana na utabiri wake.” 199Ibid., pp. 74,75.TK 208.2

  Alipogundua kuwa mtiririko wa vipindi vya matukio unafika hadi wakati wa kuja kwa Yesu mara ya pili, alihesabu kuwa “muda uliotengwa kabla” ambao Mungu aliwafunulia watumishi wake. “Mambo yale yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele”. Bwana alitamka kwamba, hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” Kum. 29:29; Amo. 3:7. Wanafunzi wa Neno la Mungu wanaweza kutazamia kukutana na matukio makubwa katika historia ya mwanadamu yakioneshwa katika Maandiko.TK 208.3

  “Nilikuwa nimekubali kabisa” alisema Miller, kuwa kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho; kwa kuwa liliandikwa na watu walioongozwa na Roho Mtakatifu, na liliandikwa kwa mafundisho ili sisi kupitia subira na faraja ya Maandiko tupate tumaini Nilijisikia kuwa katika kujitahidi kufahamu kile Mungu alichokifunua kwetu kwa neema yake, sikuwa na haki kuruka vipindi vya unabii.” 200Ibid. Unabii ulioonekana kufunua vizuri zaidi ujio Wakristo mara ya pili ni ule wa Daniel 8:14 “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifii patakapotakaswa.” Akiacha Maandiko yajitafsiri yenyewe, Miller alijifunza kuwa siku katika lugha ya mafumbo ya unabii huwakilisha mwaka mmoja. (Angalia Kiambatisho) Aliona kuwa siku za kiunabii 2300, au miaka halisi, ungeenda mbali zaidi ya kipindi cha kufungwa kwa mfumo wa dini wa Kiyahudi, kwa hiyo haikumaanishawa patakatifu pa mfumo huo.TK 208.4

  Miller aliukubali mtazamo wa jumla kuwa katika zama za Ukristo dunia ndipo “patakatifu” na kwa hiyo akaelewa kuwa kutakaswa kwa patakatifu kulikotabiriwa katika Daniel 8:14 kuliwakilisha utakaso wa dunia kwa moto wakati wa kuja kwake Kristo. Kama muda sahihi wa kuanza kwa siku 2300, ungefahamika, alihitimisha kuwa muda wa kurudi kwa Yesu mara ya pili ungekuwa umefunuliwa.TK 209.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents