Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ujumbe Uliotolewa kwa Wakati Mwafaka

    Vivyo hivyo Miller na wenzake walitimiza unabii na kutoa ujumbe uliokuwa umetabiriwa kuwa ilipasa utolewe kwa ulimwengu. Wasingeweza kuutoa ujumbe huo kama wangekuwa wameuelewa kikamilifu unabii uliokuwa unatabiri kuvunjika kwa matumaini yao na kuwasilisha ujumbe mwingine uliopasa kuhubiriwa kwa mataifa yote kabla ya kuja kwa Bwana. Ujumbe wa malaika wa kwanza na ujumbe wa malaika wa pili ulitolewa kwa wakati sahihi na ulifanya kazi ambayo Mungu alikuwa amekusudia kuifanya kwa ujumbe huo.TK 253.2

    Ulimwengu ulikuwa unatarajia kuwa kama Kristo asingerudi, imani ya Ujio ingeachwa. Lakini, pamoja na wengi kuiacha imani yao, kulikuwa na baadhi ambao walisimama imara. Matokeo ya harakati za Ujio, moyo wa kujipeleleza moyoni, wa kuikana dunia na matengenezo ya maisha, vilishuhudia kwamba jambo hili lilikuwa la Mungu. Hawakuthubutu kukanusha kwamba Roho Mtakatifu alikuwa amehusika katika mahubiri ya Ujio wa pili. Hawakuweza kugundua kosa lo lote katika vile vipindi vya unabii. Wapinzani wao walikuwa hawajafaulu kuupinga ufasiri wao. Hawakukubali kukana msimamo uliokuwa umefikiwa kwa usomaji makini wa Maandiko ulioambatana na maombi ambao ulifanywa na watu waliokuwa wameangaziwa na Roho wa Mungu na mioyo iliyokuwa ikiwaka kwa nguvu yake ihuishayo, na ambayo ilisimama imara dhidi ya elimu na lugha ya ushawishi.TK 253.3

    Waadventista walikuwa wanaamini kuwa Mungu alikuwa amewaongoza kutoa onyo juu ya hukumu. Walikuwa wanasema, “Onyo hilo limeipima mioyo ya wale waliolisikia, ... ili wale watakaojipileleza mioyo yao, wajue wangekutwa wakiwa upande gani, kama Bwana angekuja—kama wangesema ‘Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, ndiye tuliyemngoja atusaidie; huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, na tushangilie na kuufurahia wokovu wake;’ au wangeiambia miamba na milima iwaangukie ili iwasitiri mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi.” (Isaya 25:9; Ufunuo 6:16). 225The Advent Herald and Signs of the Times Reporter, vol. 8, no. 14 (Nov. 13, 1844).TK 254.1

    Hisia za wale wakuwa wanaendelea kuamini kuwa Mungu ameongoza zinaonekana katika maneno ya William Miller: “Tumaini langu la Ujio Wakristo ni imara kama lilivyokuwa siku zote. Nilichokifanya ni kile ambacho, niliona kuwa kilikuwa wajibu wangu kukifanya, baada ya kutafakari kwa makini.” “Kwa mtazamo wa kibinadamu, mahubiri yaliyokuwa yanahusu huo wakati, yaliwafanya maelfu ya watu, kusoma Maandiko; na kwa njia hiyo, wameweza kupatanishwa na Mungu kwa kunyunyiziwa damu ya Kristo.” 226Bliss, pp. 256, 255, 277, 280, 281.TK 254.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents