Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuamriwa Kwenda Gerezani na Kufa

  Kwa mara nyingine dhoruba ya hasira ilifumuka, na Jerome alipelekwa haraka gerezani. Hata hivyo wapo ambao kwao maneno yake yalikuwa yameweka mguso wa ndani sana na walitamani kuokoa maisha yake. Alitembelewa na waheshimiwa na wakamsihi ajisalimishe kwa baraza. Ahadi za kupendeza zilitajwa kwake kama zawadi.TK 74.2

  “Nihakikishieni kutoka kwenye Maandiko Matakatifu kama nimekosea,” alisema, “nami nitakana mafundisho haya.”TK 74.3

  “Maandiko Matakatifu!” mmoja wa waliomjaribu alisema kwa sauti, “inapasa tufanye kila kitu kulingana na hayo? Ni nani awezaye kuyaelewa basi hadi kanisa limeyafasiri?”TK 74.4

  Jerome akamjibu: “Je, mapokeo ya wanadamu ni ya thamani katika imani kuliko Injili ya Mwokozi wetu?”TK 74.5

  “Mzushi!” ndilo lililokuwa jibu la mmoja wao, “Ninajuta kwa kubembelezana nawe kwa muda mrefu kiasi hiki. Ninaona umetiwa moyo na mwovu.” 30Wylie, bk. 3, ch. 10.TK 74.6

  Baada ya muda mfupi, alipelekwa hadi mahali pale pale ambapo Huss alitoa uhai wake. Alikwenda akiimba njiani, uso wake uking’azwa kwa furaha na amani. Kwake yeye mauti imepoteza utisho wake. Wakati mnyongaji alipokuwa tayari kuuwasha moto, alipokaribia nyuma yake, mfia dini alisema kwa sauti, “Weka moto usoni mwangu. Ningekuwa na hofu, nisingekuwa hapa.”TK 74.7

  Maneno yake ya mwisho yalikuwa sala: “Bwana, Baba Mwenyezi, nihurumie, unisamehe dhambi zangu; kwani wewe unajua kuwa daima nimeupenda ukweli wako.” 31Bonnechose, vol. 2, p. 168. Majivu ya mfia dini yalikusanywa, na kama yalivyokuwa yale ya Huss, yalitupwa kwenye mto Rhine. Hivyo ndivyo walivyokufa wajumbe wa Mungu waaminifu walioibeba nuru.TK 74.8

  Kuuawa kwa Huss kulikuwa kumeibua moto wa ghadhabu na utisho katika Bohemia. Taifa zima lilikuwa limemtangaza kuwa mwalimu mwaminifu wa ukweli. Baraza likashitakiwa kwa kuua. Mafundisho yake yakaweka mvuto mkubwa kuliko wakati uliopita, na wengi wakaongozwa kukubali imani ya matengenezo. Papa na mfalme waliungana ili kulizima vuguvugu hili, na majeshi ya Sigismund yakamwagwa Bohemia.TK 75.1

  Lakini mkombozi aliinuliwa. Ziska, mmoja kati ya majenerali waliokuwa na uwezo sana wa wakati wake, alikuwa ndiye kiongozi watu wa Bohemia. Akitegemea msaada wa Mungu, watu wale waliweza kupambana dhidi ya jeshi lililokuwa na nguvu sana kuliko yote ambayo yangewakabili. Kwa kurudia rudia, mfalme aliivamia Bohemia, na akaishia kurudishwa nyuma. Wafuasi wa Huss waliinuliwa juu ya hofu ya mauti, na hakuna ambacho kingewapinga. Shujaa Ziska alikufa, lakini mahali pake pakachukuliwa na Procopius, kwa namna fulani akiwa kiongozi mwenye uwezo zaidi.TK 75.2

  Papa akatangaza mashambulio dhidi ya wafuasi wa Huss. Nguvu kubwa kuliko kawaida ilipelekwa kwa haraka Bohemia, na bado walishindwa vibaya. Shambulio lingine lilitangazwa. Katika nchi zote zilizokuwa kwenye mamlaka ya Papa kule Ulaya; watu, fedha na silaha za vita vilikusanywa. Umati wa watu ulijiunga na bendera ya Papa.TK 75.3

  Nguvu kubwa sana ya kijeshi iliingia Bohemia. Watu walikusanyika ili kuwarudisha nyuma. Majeshi mawili yalikaribiana hadi ikawa ni mto tu ulioyatenganisha. “Washambuliaji walikuwa na jeshi kubwa na bora zaidi, lakini badala ya kuvuka mto, ili kukamilisha pambano dhidi ya wafuasi wa Huss, ambao walikuwa wamekuja mwendo wote huo ili kupambana nao, walisimama kimya wakiwaangalia wale mashujaa.” 32Wylie, bk 3, ch. 17.TK 75.4

  Ghafla, jambo kubwa la kutisha lililiangukia jeshi. Bila hata ya pigo moja, jeshi lile kubwa lilivunjika na kutawanyika kana kwamba lilitawanywa na nguvu isiyoonekana. Jeshi la wafuasi wa Huss liliwakimbiza hawa waliokuwa wakitoroka, na vitu vingi vilivyotekwa vikakamatwa na washindi. Kwa hiyo vita, badala ya kuwafanya Wabohemia kuwa fukara, viliwatajirisha.TK 75.5

  Miaka michache baadaye, chini ya Papa mpya, shambulio lingine liliandaliwa. Jeshi kubwa likaingia Bohemia. Majeshi ya wafuasi wa Huss yalirudi nyuma mbele yao, hivyo, wavamizi wakaingia ndani zaidi katika nchi, jambo lililowafanya wafikiri wamekwisha kushinda.TK 76.1

  Hatimaye, jeshi la Procopius lilisonga mbele ili kupambana nao. Sauti ya jeshi lililokaribia iliposikika, hata kabla wafuasi wa Huss hawajaonekana, hofu iliwajaza wavamizi tena. Wana wa kifalme, majenerali, na askari wa kawaida, huku wakizitupa silaha zao, walikimbia na kutawanyika pande zote. Ushindi ulikuwa kamili, na kwa mara nyingine tena nyara nyingi sana zikaingia mikononi mwa washindi.TK 76.2

  Kwa namna hiyo, kwa mara ya pili jeshi ia watu wa vita, waliofundishwa kwa ajili ya mapambano, walikimbia bila ya kupigwa mbele za walinzi wa taifa dogo dhaifu. Wavamizi walipigwa kwa utisho wa yeye aliye na nguvu isiyo ya kibinadamu. Yeye aliyewakimbiza majeshi ya Wamidiani mbele za Gideoni na watu wake mia tatu, alikuwa amenyoosha tena mkono wake. Angalia Amu. 7:19-25; Zab.53:5.TK 76.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents