Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuishika Jumapili

  Kuishika Jumapili ni desturi iliyoanzishwa na Kanisa la Roma, ambalo linadai kama ndiyo alama ya mamlaka yake. Roho ya utawala wa Papa - ya kuzikubali desturi za kidunia, kuzitukuza mila za wanadamu kupita amri za Mungu-inapenya ndani ya makanisa ya Kiprotestanti na kuwaongoza kwenye kazi ile ile ambayo utawala wa Papa uliifanya kabla yao; ya kuiinua Jumapili.TK 348.2

  Sheria za kifalme, mabaraza makuu, na sheria za kanisa zikisaidiwa na nguvu ya serikali zilikuwa ni hatua zilizowezesha sherehe za kipagani kupata nafasi ya heshima kwenye ulimwengu wa Ukristo. Hatua ya kwanza ya kulazimishwa ushikajiji wa Jumapili kwa watu wote, ni sheria iliyowekwa na Kostantino. Ingawa kimsingi ni sheria ya kipagani, ilikuwa imelazimishwa na mfalme baada ya kuupokea Ukristo kwa jina tu.TK 348.3

  Eusebio, askofu aliyetafuta kupendwa na wakuu, na ambaye alikuwa rafiki wa pekee wa Kostantino, alilieneza dai kuWakristo alihamisha Sabato kwenda Jumapili. Hakuna ushuhuda wa Maandiko unaotolewa kulihakikisha hilo. Eusebio mwenyewe pasipo kujua anakiri hilo si halali. “Mambo yote” anasema, jambo lolote lililokuwa ni wajibu kutendwa siku ya Sabato, tumelihamisha kwenda kwenye Siku ya Bwana” 236Robert Cox, Sabhath Laws and Sabbath Duties, p. 538 Utawala wa Papa ulipoanzishwa, Jumapili iliendelea kuinuliwa. Kwa muda fulani siku ya saba iliendelea kuchukuliwa kama ndiyo Sabato, lakini polepole badiliko lilifanyika. Baadaye Papa alitoa maelekezo kwamba paroko anapaswa kuwaonya wanaokiuka kutunza Jumapili wasije wakapata madhara makubwa wao na majirani zao.TK 348.4

  Maagizo ya mabaraza yaliposhindwa, mamlaka za serikali ziliombwa kutoa sheria ambayo ingetia hofu ndani ya mioyo ya watu na kuwalazimisha kuacha kufanya kazi siku ya Jumapili. Katika mkutano wa majimbo (sinodi) uliofanyika Roma, uamuzi wote uliotangulia ulisisitizwa upya na kujumuishwa kwenye sheria za kanisa na kulazimishwa na mamlaka za umma. 237Heylyn, History of the Sabbath, pt. 2, ch. 5, sec. 7.TK 349.1

  Hali ya kuutokuwepo kwa mamlaka ya Maandiko inayoagiza kushika Jumapili bado ilikuwa inaleta usumbufu. Watu walikuwa wanauliza juu ya haki ya walimu wao kuliweka kando tangazo, “Siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako.” ili kuiheshimu siku ya jua. Ili kujaza nafasi ya kutokuwepo ushuhuda wa Biblia, kukawa na ulazima wa kuweka sababu zilizokuwa zinaonekana kufaa.TK 349.2

  Mtetezi wa Jumapili mwenye bidii, ambaye mwishoni mwa kame ya kumi na mbili alitembelea makanisa ya Uingereza, alikataliwa na mashahidi waaminifu wa ukweli; na hivyo juhudi zake hazikuzaa matunda na akaondoka huko kwa muda. Aliporejea, alikuwa na gombo alilodai kuwa lilitoka kwa Mungu mwenyewe, ndani yake lilikuwa na amri iliyohitajika ya kushika Jumapili, ikiambatana na vitisho vikubwa kuwapa hofu ambao wangekataa kutii. Waraka huo wa thamani inasemekana ulianguka kutoka mbinguni na uliokotwa Yemsalemu juu ya madhabahu ya Mtakatifu Simeoni, huko Goligota. Lakini kwa hakika ikulu ya Papa huko Roma ilikuwa ndiyo chanzo chake. Udanganyifu na mambo ya kughushi katika vizazi vyote yamekuwa yakihalalishwa na utawala wa Papa. (Angalia Kiambatisho)TK 349.3

  Lakini bila kujali jitihada zote za kuuimarisha utakatifu wa Jumapili, Wakatoliki wenyewe walikiri hadharani kuwa Sabato inayo mamlaka kutoka kwa Mungu. Katika kame ya kumi na sita baraza la kiPapa lilitangaza kuwa, “Hebu Wakristo wote wakumbuke kuwa Sabato ilitakaswa na Mungu, na imekuwa ikipokelewa na kutunzwa, siyo tu na Wayahudi, lakini na wote wengine waliokuwa wanajifanya kumwabudu Mungu; ingawa Wakristo waliibadili Sabato yao kwenda kwenye Siku ya Bwana.” 238Thomas Morer, Discourse in Six Dialogues on the Name, Notion, and Observation of the Lord’s Day, pp. 281, 282. Wale waliokuwa wanajaribu kuibadili sheria ya Mungu hawakuwa gizani juu ya tabia ya kazi yao.TK 349.4

  Kielelezo cha kuvutia juu ya sera ya Kanisa la Roma kilitolewa wakati wa mateso ya muda mrefu yenye umwagaji damu dhidi ya Wawaldensia, baadhi yao wakiwa watunza Sabato. (Angalia Kiambatisho) Historia ya makanisa ya Ethiopia na Abyssinia ni ya muhimu. Katikati ya utusitusi wa Zama za Giza, Wakristo wa Afrika ya kati hawakujulikana na walikuwa wamesahauliwa na ulimwengu na kwa kame nyingi walifurahia uhuru wa Ukristo wao. Mwishowe Kanisa la Roma likagundua uwepo wao, na mfalme wa Abyssinia akadanganywa na kumtambua Papa kama wakili Wakristo. Sheria ilitangazwa ya kukataza utunzaji wa Sabato, ikiambatana na adhabu kali. 239Michael Geddes, Church History of Ethiopia, pp. 311,312. Lakini ghafla udhalimu wa Papa ukawa kama nira inayoumiza hata watu wa Abyssinia wakaazimu kuivunja. Wakatoliki walipigwa marufuku kwenye utawala wao na imani yao ya awali ikarejeshwa.TK 350.1

  Wakati ambapo makanisa ya Afrika yalikuwa yanatunza Sabato na kuzitii amri za Mungu, hawakufanya kazi siku ya Jumapili kulingana na desturi za kanisa. Kanisa la Roma liliikanyaga sheria ya Mungu na kuiinua sheria yake, lakini makanisa ya Afrika, yakiwa yamefichwa kwa karibu miaka elfu moja, hayakushiriki uasi huu. Yalipowekwa chini ya Kanisa la Roma, yalilazimishwa kuiweka kando Sabato ya kweli na kuiinua ya uongo. Lakini mapema baada ya kupata uhuru wao walirudia kwenye utii wa amri ya nne. (Angalia Kiambatisho)TK 350.2

  Kumbukumbu hizi zinafunua kwa uwazi uadui wa Kanisa la Roma dhidi ya Sabato na Watetezi wake. Neno la Mungu linatufundisha kuwa matukio haya yatajirudia wakati Ukatoliki utakapoungana na Uprotestanti kwa ajili ya kuiinua Jumapili.TK 350.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents