Sura Ya 23 - Fumbo Lililo Wazi La Patakatifu
Andiko lililokuwa msingi na nguzo ya imani ya Waadventista ni tangazo lisemalo, “Hata nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.” Danieli 8:14. Haya yalikuwa maneno ya kawaida kwa wote waliokuwa wanaamini kuwa Bwana alikuwa anakuja upesi. Lakini Bwana alikuwa hajatokea. Wale waumini walikuwa wanaamini kuwa Neno la Mungu lisingesema uongo; bila shaka ufasiri wao wa unabii ulikuwa na kasoro. Lakini kasoro ilikuwa wapi?TK 256.1
Mungu alikuwa wamewaongoza watu wake katika harakati kubwa za Ujio. Asingeruhusu ziishie katika giza na kuvunjika moyo, zikishutumiwa kuwa za uongo na zenye itikadi kali. Ingawa wengi waliachana na hesabu zao za vipindi vya uabii na kuzikana harakati hizo kwa sababu hiyo, wengine hawakuwa tayari kuzikana hoja za imani na matukio ambayo yalithibitishwa na Maandiko pamoja na Roho wa Mungu. Ulikuwa wajibu wao kushikilia ulweli uliokuwa umekwisha kupatikana. Waliyachunguza Maandiko kwa maombi ya dhati ili waone kosa lao. Walipoona kuwa hakukuwa na kosa katika hesabu zao za vipindi vya unabii, walianza kuchunguza kwa undani zaidi suala la patakatifu.TK 256.2
Waligundua kuwa hakukuwa na ushahidi wa Maandiko unaounga mkono dhana ya wengi kwamba dunia ndiyo patakatifu; bali walipata maelezo kamili ya patakatifu, palivyo, pako wapi na huduma zake; “Basi hata agano la kwanza lilikuwa na kawaida za ibada, na patakatifu pake, pa kidunia. Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho; ndipo palipoitwa, patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo patakatifu pa patakatifu, yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na ile fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; na juu yake makerubi ya utukufu, yakikitia kivuli kiti cha rehema; basi hatuna nafasi sasa ya kueleza habari za vitu hivi kimoja kimoja.” Waebrania 9:1-5.TK 256.3
Patakatifu palikuwa mahali palipojengwa na Musa kwa agizo la Mungu kama makazi ya Aliye Juu hapa duniani. Agizo alilopewa Musa lilikuwa “Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao” (Kutoka 25:8). Hema ile ilikuwa jengo lenye utukufu. Pamoja na ua wa nje, hema yenyewe ilikuwa na vyumba viwili vilivyokuwa vinaitwa patakatifu na patakatifu sana, vilivyokuwa vinatenganishwa na pazia. Pazia la aina hiyo hiyo lilikuwa linaziba mlango wa kuingilia katika chumba cha kwanza.TK 257.1