Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sura Ya 28 - Kukabiliana Na Kumbukumbu Ya Maisha Yetu

  “Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” Danieli 7:9, 10.TK 296.1

  Hivi ndivyo Danieli alivyopewa maono ya ile siku kuu wakati maisha ya wanadamu yatakapochunguzwa mbele ya hakimu wa dunia yote. Mzee wa Siku ni Mungu Baba. Yeye, aliye asili ya viumbe vyote, chemchemi ya sheria yote, ndiye atakayeongoza hukumu. Na malaika watakatifu watakuwa watumishi na mashahidi.TK 296.2

  “Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele.” Danieli 7:13, 14.TK 296.3

  Kuja kwa Kristo kunakoelezewa hapa, siyo tukio la kuja kwake mara ya pili duniani. Anakuja kwa Mzee wa Siku mbinguni ili apokee ufalme atakaopewa mwishoni mwa kazi yake kama mpatanishi. Ni tukio hili, na siyo, kuja kwake duniani mara ya pili, ambalo lilikuwa linakwenda kutimia mwishoni mwa unabii wa siku 2300 hapo mwaka 1844. Kuhani wetu mkuu aliingia Patakatifu sana ili afanye sehemu ya mwisho ya huduma ya upatanisho kwa niaba ya wanadamu.TK 296.4

  Katika huduma kielelezo(patakatifu pa duniani), ni wale tu ambao dhambi zao zilikuwa zimepelekwa kwenye hema ya kukutania, waliokuwa na sehemu katika Siku ya Upatanisho. Vivyo hivyo katika siku kuu ya upatanisho na hukumu ya upelelezi mashauri yanayotendewa kazi ni ya wale tu wanaodai kuwa watu wa Mungu. Hukumu ya waovu ni kazi itakayofanyika baadaye. “Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu. 1 Petro 4:17.TK 296.5

  Vitabu vya kumbukumbu vilivyoko mbinguni ndivyo vitakavyotumika kufanya uamuzi. Kitabu cha uzima kina majina ya wale wote waliowahi kufanya kazi ya Mungu. Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni.” Paulo anawaambia Watendakazi wenzake, “majina yao yamo katika kitabu cha uzima.” Danieli anasema kuwa watu wa Mungu wataokolewa “kila mmoja atakayeonekana ameandikwa katika kitabu kile.” Na Yohana wa Ufunuo anasema watakaoingia katika mji wa Mungu ni wale wenye majina, “Yaliyoandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo.” Luka 10:20; Wafilipi 4:3; Danieli 12:1; Ufunuo 21:27.TK 297.1

  Kwenye “Kitabu cha kumbukumbu” yameandikwa matendo mema ya “Hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake.” Kila jaribu walilolipinga, kila uovu walioushinda, kila neno la huruma lililotolewa, kila tendo la kujitoa, kila uchungu uliovumiliwa kwa ajili ya Yesu vimeandikwa. “Umehesabu kutanga-tanga kwangu; Uyatie machozi yangu katika chupa yako; (Je! Hayamo katika kitabu chako?)” Malaki 3:16; Zaburi 56:8.TK 297.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents