Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utakaso Unaotajwa Kwenye Biblia

  Utakaso unapaswa kuwa kamili unaojumuisha roho, nafsi, na mwili. (Angalia, 1 Wathesalonike 5:23). Wakristo wanatakiwa kuitoa miili yao, “iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu” Warumi 12:1. Kila tendo linalodhoofisha nguvu za mwili au za akili linamwondolea mwanadamu sifa za kumhudumia Mwumbaji wake. Wale wanaompenda Mungu kwa moyo wote watadumu kujitahidi kuweka kila nguvu waliyonayo ipatane na sheria zinazowapa uwezo wa kufanya mapenzi yake. Hawatadhoofisha ama kuinajisi sadaka wanayoitoa kwa Baba yao wa mbinguni; kwa kuendekeza uchu na tamaa za mwili.TK 292.5

  Kila tendo la kujifurahisha kwa dhambi huelekea kupumbaza na kufisha utambuzi wa kiakili na wa kiroho; moyo huvutiwa kidogo mno na Neno au Roho wa Mungu. “Na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.” 2 Wakorintho 7:1.TK 293.1

  Ni wangapi wanaokiri kuwa Wakristo; ambao wanaushusha ubinadamu wao wenye mfano wa Mungu kwa ulafi, kwa kunywa pombe, na kwa anasa zisizoruhusiwa. Na mara nyingi kanisa linahamasisha uovu, ili kutunisha hazina yake ambayo upendo kwa Kristo ulio duni ndani yao umeshindwa kuijaza. Endapo Yesu angeingia kwenye makanisa ya leo na kuziangalia sikukuu zinazoendeshwa kama za kidini; je, hangewafukuza hao waharibifu wa vitu vitakatifu kama alivyowafanyia wavunja fedha hekaluni? “Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.” 1 Wakorintho 6:19, 20. Yule ambaye mwili wake ni hekalu la Roho hawezi kuwa mtumwa wa tabia zenye madhara. Uwezo wake wote unamilikiwa na Kristo. Mali yake ni ya Bwana. Atawezaje kutapanya mtaji alioaminiwa na Bwana?TK 293.2

  Wale wanaokiri kuwa Wakristo kila mwaka hugharamia na kuzika pesa nyingi kuridhisha uchu kwa vitu vinavyodhuru. Mungu ameibiwa zaka na sadaka. Wao wanatumia, kwa ajili ya tamaa, zaidi ya vile ambavyo wangetoa kusaidia maskini au kusaidia kazi ya Injili. Matokeo ni uangamivu. Kama wote wanaomkiri Kristo wangekuwa wametakaswa kweli kweli, mali zao, zingepelekwa kwenye hazina ya Bwana, badala ya kutumika kwa vitu visivyo vya lazima vyenye kutosheleza uchu na mwisho vina madhara. Wakristo wangeweka kielelezo kwa kuwa na kiasi na kujitoa kafara nafsi zao. Ndipo watakuwa nuru ya Ulimwengu.TK 293.3

  “Tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima” (1 Yohana 2:16), huwatawala watu wengi. Lakini wafuasi Wakristo wana mwito mtakatifu. “Tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema Bwana, msiguse kitu kilicho kichafu” Kwa wale wanaoenenda sawa na masharti hayo, ahadi ya Mungu ni, “Nitakuwa Baba kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike” 2 Wakorintho 6:17, 18.TK 294.1

  Kila hatua ya imani na utii inauleta moyo karibu na muunganiko na Yeye aliye nuru ya ulimwengu. Miali angavu ya Jua la Haki huwaangazia watumishi wa Mungu, wao wanapaswa kuakisi miali hiyo. Nyota zinatuambia kuwa kuna nuru mbinguni ambayo utukufu wake unazifanya zing’ae; vivyo hivyo Wakristo wanadhihirisha kuwa yuko Mungu kwenye kiti cha enzi, ambaye tabia yake inastahili kutukuzwa na kuigwa. Utakatifu wa tabia yake utadhihirika ndani ya mashahidi wake.TK 294.2

  Kupitia sifa njema za Kristo tunayo njia ya kukifikia kiti cha enzi cha Uwezo usio na kikomo. “Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?” “Ombeni, nanyi mtapata”; furaha yenu iwe timilifu. Yesu anasema: “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?” “Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.” Warumi 8:32; Luka 11:13; Yohana 14:14; 16:24.TK 294.3

  Ni fursa ya kila mmoja kuishi hivyo ili Mungu ampe kibali na ambariki. Siyo mapenzi ya Baba yetu wa mbinguni kwamba tutakuwa daima chini ya hukumu na giza. Hakuna ushahidi juu ya unyenyekevu wa kweli unaoonekana kwa mtu kutembea akiinamaisha kichwa na moyo uliojaa mawazo ya ubinafsi. Tunaweza kwenda kwa Yesu akatutakasa na kusimama mbele ya sheria bila aibu wala huzuni.TK 294.4

  Kwa njia ya Yesu, wana wa Adamu walioanguka wanakuwa, “wana wa Mungu.” “Haoni haya kuwaita ndugu zake” Maisha ya Mkristo yapaswa kuwa yale ya imani, ushindi na furaha katika Mungu. “Furaha ya Bwana ni nguvu zenu.” “Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.” Waebrania 2:11; Nehemia 8:10; 1 Wathesalonike 5:16-18.TK 294.5

  Haya ndiyo matunda ya uongofu na utakaso unaofundishwa ndani ya Biblia; matunda haya yanashuhudiwa mara chache kwa sababu, kanuni kuu za haki zilizowekwa zimeachwa bila kujali. Na ndiyo maana ule udhihirisho wa kina, wa kazi ya kudumu ya Roho Mtakatifu, ambao ulionekana kwenye uamsho wa zamani, upo kidogo sana.TK 295.1

  Ni kwa kutazama ndipo tunapobadilika. Kwa kadiri yale maagizo matakatifu ambamo Mungu amewafunulia wanadamu ukamilifu na utakatifu wa tabia yake yanavyochwa; na akili za watu zikivutiwa na mafundisho ya watu na nadharia zao; kumekuwepo na upungufu katika uchaji wa Mungu ndani ya kanisa. Ni pale tu sheria ya Mungu itakaporejeshwa mahali pake sahihi; ndipo utakapokuwepo uamsho wa imani ya zamani na utauwa miongoni mwa watu wanaomkiri.TK 295.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents