Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuitafuta Amani

  Shauku ya kutafuta amani kati yake na Mungu ilikuwa inamwongoza kujitoa mwenyewe kuishi maisha ya kitawa. Hapa alikuwa anatakiwa kufanya kazi duni za kuchosha na kuombaomba nyumba kwa nyumba. Kwa ustahimilivu alivumilia hali hiyo duni, akiamini kuwa ilikuwa ni lazima kufanya hivyo kwa sababu ya dhambi zake.TK 79.3

  Alikuwa anajinyima usingizi na kuwa na chuki hata wakati wa milo yake iliyokuwa haitoshi, ili afurahie kujifunza Neno la Mungu. Aliiona Biblia imefungwa kwa minyororo kwenye ukuta wa nyumba ya watawa, na hili alilisema mara kwa mara.TK 79.4

  Alikuwa anaishi maisha magumu sana, akijitahidi kwa kufunga, kukosa usingizi, na kujitesa ili kudhibiti uovu wake. Baadaye alisema, “Ikiwa mtawa ataingia mbinguni kwa njia ya kazi zake za kitawa, kwa hakika ningestahili nafasi hiyo...kama ningeendelea kwa muda mrefu zaidi, ningeweza kuudhalilisha mwili wangu hadi mauti.” 37Ibid., ch. 3. Pamoja na jitihada hizo zote, roho yake iliyokuwa imeelemewa haikupata ahueni. Hatimaye alifika kwenye ukingo wa kukata tamaa.TK 79.5

  Ilipoonekana kwamba kila kitu kilikuwa kimepotea, Mungu akamwinua rafiki kwa ajili yake. Staupitz alilifungua Neno la Mungu kwenye akili ya Luther na kumtaka asiiangalie nafsi bali amwangalie Yesu. “Badala ya kujitesa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zako, jitupe kwenye mikono ya Mwokozi. Mwamini, iamini haki iliyo katika maisha yake, katika upatanisho wa kifo chake...Mwana wa Mungu...alifanyika mwanadamu ili akupatie uhakika wa kibali cha Mungu...mpende ambaye alikupenda kwanza.” 38Ibid., ch. 4. Maneno yake yalileta mvuto wa kina ndani ya moyo wa Luther. Amani ikaja ndani ya nafsi iliyokuwa inataabika.TK 80.1

  Baada ya kuwekewa mikono ya upadre, Luther aliitwa kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Wittenberg. Alianza kutoa mihadhara juu ya Zaburi, Injili, na Nyaraka kwenye makundi ya wasikilizaji wenye furaha. Staupitz, mkubwa wake, alimtaka apande mimbarani kuhubiri. Lakini Luther alikuwa anajihisi kutostahili kuzungumza na watu kwa niaba ya Kristo. Ilikuwa baada ya masumbuko ya muda mrefu na rafiki zake wakimsihi, ndipo alipokubali. Alikuwa na nguvu katika Maandiko, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Usahihi na uwezo aliotumia kuuwasilisha ukweli, vilishawishi ufahamu wao na hamasa yake iliigusa mioyo yao.TK 80.2

  Akiwa bado mwana wa kweli wa Kanisa la Papa, Luther hakuwa na wazo kwamba angekuwa mtu tofauti. Alipoongozwa kwenda Roma, aliishika njia kwa safari ya miguu, alikuwa analala kwenye nyumba za watawa njiani. Alistaajabia uzuri na anasa alizozishuhudia. Watawa walikuwa wanaishi katika nyuumba nzuri za fahari, walikuwa wanavaa mavazi ya thamani kubwa, walikuwa wanafanya karamu zao kwenye meza za gharama kuu. Moyo wa Luther ulianza kupata mashaka.TK 80.3

  Hatimaye kwa mbali aliuona ule mji wa vilima saba. Alianguka kifudifudi hadi chini ya nchi, akistaajabu na kusema: “Roma Mtakatifu, Ninakusalimu!” 39 Ibid., bk. 2, ch.6. Aliyatembelea makanisa, akazisikiliza hadithi za kuvutia zilizorudiwa mara kwa mara na mapadre na watawa, na akatimiza zile ibada zilizokuwa zinatakiwa. Kila mahali, matukio yalimfanya kushangaa-uovu miongoni mwa mapadre, na utani usio na maana kutoka kwa maaskofu. Alitishwa na machafu hata kwenye ibada. Alikutana na ufujaji, mauaji. “Hakuna awezaye kufikiria,” aliandika, “ni dhambi na matendo maovu ya namna gani yanayotendeka Roma...wamezoea kusema kuwa, ‘kama kuna jehanamu, basi Roma imejengwa juu yake.’40Ibid.TK 81.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents