Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kukutana kwa Adamu Wawili

  Waliokombolewa watakapokuwa wakikaribishwa katika mji wa Mungu, hapo itasikika kelele ya ushindi. Adamu wawili karibia wanakutana. Mwana wa Mungu atampokea baba wa jamii yetu-ambaye alimuumba, aliyetenda dhambi, na kwa sababu ya dhambi yake alama za kusulubishwa ziko kwenye mwili wa Mwokozi. Adamu atakapokuwa akiziangalia alama za misumari, kwa unyenyekevu ataanguka miguuni pa Mwokozi. Mwokozi atamwinua na kumkaribisha aiangalie bustani ya Edeni ambayo aliondolewa kutoka kwayo muda mrefu.TK 387.2

  Maisha ya Adamu yalikuwa yamejaa huzuni. Kila jani lililoanguka, kila mnyama wa kafara, kila doa katika maisha safi ya mwanadamu ulikuwa ni ukumbusho wa dhambi yake. Alikuwa na uchungu na majuto ya kutisha alipokutana na shutuma alizotupiwa yeye kama aliyesababisha dhambi. Kwa uaminifu alitubu dhambi yake, na alikufa katika tumaini la ufufuo. Sasa kupitia katika upatanisho, Adamu atakuwa amerejeshwa.TK 387.3

  Atasafirishwa kwa furaha, ataiona miti ambayo hapo awali ilikuwa furaha yake, ambayo matunda yake yeye mwenyewe aliyachuma katika siku zile ambazo alikuwa hana hatia. Ataiona miti ambayo aliihudumia kwa mikono yake, maua yale yale aliyokuwa akipenda kuyatunza. Kwa hakika hii ni Edeni iliyorejeshwa!TK 387.4

  Mwokozi atampeleka kwenye mti wa uzima na kumsihi ale. Atayaona makutano ya familia yake wakiwa wamekombolewa. Kisha atatupa taji yake miguuni pa Yesu na kumkumbatia Mwokozi. Atashika kinubi na anga la mbinguni litakuwa na mwangi wa wimbo wa ushindi: “Astahili Mwana-Kondoo aliyechinjwa.” Ufunuo 5:12. Familia ya Adamu watatupa taji zao miguuni pa Yesu watakaposujudu kumtukuza. Malaika walilia Adamu alipoanguka na walifurahi Yesu alipolifungua kaburi kwa wote watakaoliamini Jina lake. Sasa wataiangalia kazi ya ukombozi ikiwa imekamilishwa na kuunganisha sauti zao katika kusifu.TK 387.5

  Kwenye “bahari ya kioo iliyochangamana na moto,” watakusanyika wale “wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake.” Mia moja arobaini na nne elfu waliokombolewa kati ya watu na wanaimba “wimbo mpya” wimbo wa Musa na Mwana- Kondoo. Ufunuo 15:2,3. Si wengine isipokuwa wale mia moja arobaini na nne elfu ndio watakaoweza kujifunza wimbo ule, kwa sababu ni wimbo wa uzoefu ambao hamna kundi lingine wamewahi kuupitia. “Hawa ndio wamfuatao Mwana-Kondoo kila aendako.” Hawa baada ya kubadilishwa kutoka miongoni mwa walio hai, ni “malimbuko kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo.” Ufunuo 14:4,5. Walipitia katika kipindi cha mateso ambacho kamwe hakijawahi kuwapo tangu taifa lilipoanza kuwepo, walivumilia uchungu wa wakati wa taabu ya Yakobo, walisimama bila kuwa na mpatanishi katika kipindi cha mwisho cha hukumu ya Mungu. “nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo.” “Na katika vinywa vyao haukuonekana uongo. Maana hawana mawaa” mbele za Mungu. “Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana huyo Mwana-Kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.” Ufunuo 7:14; 14:5; 7:16,17.TK 388.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents