Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Msimamo Adilifu wa Wakuu

  Ferdinand, aliyekuwa mwakilishi wa mfalme mkuu, alijaribu kutumia ustadi wa ushawishi. “Aliwasihi wakuu walipokee agizo, akiwathibitishia kuwa mfalme mkuu angewafurahia sana.” Lakini watu hawa walimjibu kwa utulivu wakisema: “Tutamtii mfalme mkuu kwa kila jambo litakalochangia kudumisha amani na heshima kwa Mungu.”TK 130.3

  Hatimaye mwakilishi wa mfalme alitangaza ya kuwa, “njia moja tu ilikuwa imebakia kwao; kujisalimisha kwa uamuzi wa wengi.” Na aliRomaliza kusema maneno hayo aliondoka bila kuwapatia Wanamatengenezo nafasi ya kujibu. “Walituma wawakilishi ili kumsihi mfalme arudi.” Naye aliwajibu, “Ni jambo lililokwisha kuamuliwa, kutii ndiyo jambo pekee lililobakia.” 121Ibid.TK 131.1

  Upande wa mfalme ulikuwa ukijidanganya kwamba kusudio la mfalme na Papa lilikuwa thabiti na lile la Wanamatengenezo dhaifu. Iwapo Wanamatcngenezo wangetegemea msaada wa kibinadamu pekee; wasingekuwa na nguvu zozote kama wafuasi wa Kanisa la Papa walivyodhani. Lakini walikata rufaa “kutoka katika taarifa za Mkutano wa Kidini kwenda kwa Neno la Mungu, na kutoka kwa Charles mfalme kwenda kwa Yesu Kristo, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana.”TK 131.2

  Ferdinand alipokataa kuangalia kwa makini msimamo wa dhamiri zao, wakuu waliamua kumpuuza, na kupeleka hoja yao mbele ya baraza la taifa bila kuchelewa. Tamko zito lilipitishwa na kupelekwa kwenye mkutano mkuu.TK 131.3

  “Kwa hati hii tunapinga... kwa niaba yetu na watu wetu, hatuko tayari kuridhia wala kuwa waaminifu kwa namna yoyote ile katika agizo lililopendekezwa, kwa kitu chochote kilicho kinyume na Mungu, na kwa Neno lake Takatifu, na kwa dhamiri zetu sahihi, kwa ajili ya wokovu wetu...Kwa sababu hii tunaikataa nira iliyolazimishwa kwetu.TK 131.4

  ... Wakati huohuo tunategcmea kuwa, mheshimiwa mfalme atatutendea sisi kama Mkristo anayempenda Mungu kuliko kitu chochote; na sisi wenyewe tunatangaza kwamba tuko tayari kumwonesha yeye, na ninyi watawala wetu wenye neema, upendo na utii wote mambo ambayo ni haki na wajibu wetu halali.” 122Ibid. bk. 13, ch. 6.TK 131.5

  Walio wengi walijawa na mshangao na hofu kwa ujasiri wa wapinzani. Mgawanyiko, machafuko, na umwagikaji wa damu vilionekana kutoepukika. Wakiwa wameutegemea mkono wa Mungu, Wanamatengenezo “walikuwa wamejawa na ujasiri na uthabiti.”TK 131.6

  “Kanuni zilizotumika ndani ya upinzani huu mkuu ndizo zilizojenga tabia ya UprotestantL.Uprotestanti unaiweka nguvu ya dhamiri juu ya hakimu, na mamlaka ya Neno la Mungu juu ya kanisa linaloonekana...Wanasema pamoja na mitume na manabii kuwa, ‘imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.’ Mbele ya taji ya kifalme ya Charles V, wanaiinua juu taji ya Yesu Kristo.” 123Ibid. Upinzani uliofanywa kule Spires ulikuwa ni ushahidi mzito dhidi ya kutovumiliana kidini na utetezi wa haki ya watu wote kumwabudu Mungu kulingana na dhamiri zao wenyewe.TK 132.1

  Uzoefu huu wa Wanamatengenezo waadilifu ni fundisho kwa vizazi vyote vitakavyofuata. Bado Shetani anapingana na Maandiko Matakatifu kufanywa mwongozo wa maisha. Katika zama zetu kuna haja ya kurudi kwenye kanuni kuu ya Uprotesanti- yaani Biblia, na Biblia pekee kama kanuni ya imani na wajibu. Shetani bado anafanya kazi kuangamiza uhuru wa dini. Nguvu ya mpinga Kristo ambayo wapinzani wa Spires waliikataa sasa inatafuta kurudisha upya mamlaka yake iliyopoteza.TK 132.2

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents