Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kumngoja Bwana Wao

  lle kelele, “Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki” iliwafanya maelfu watarajie Ujio wa Bwana mara moja. Bwana arusi alikuja katika wakati uliopangwa, si duniani, lakini kwa Mzee wa Siku kule mbinguni, kwenye arusi, kupokea ufalme wake. “Nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini.” Haikuwapasa kuwa hapo kwani walikuwa duniani. Inawapasa wafuasi Wakristo “kumngojea Bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.” Luka 12:36. Laini inawapasa kuielewa kazi yake na kumfuata kwa imani. Kwa maana hiyo wanasemekana kuwa wamekwenda kwenye arusi. Ila inawapasa kuielewa kazi yake na kumfuata kwa imani.TK 267.2

  Katika mfano huo, wale waliokuwa na mafuta katika taa zao waliingia arusini. Wale ambao walingoja kwa uvumilivu, katika giza Ia majaribu makali, wakiichunguza Biblia kwa ajili ya nuru zaidi—hawa waliuona ukweli juu ya patakatifu pa mbinguni na badiliko la huduma ya Mwokozi. Walimfuata kwa imani katika kazi yake ya patakatifu kule juu. Na wale wote wanaoupokea ukweli huo, wakimfuata Kristo kwa imani akifanya kazi yake ya mwisho ya uombezi, wataingia katika arusi.TK 267.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents