Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mmwito wa Kumsujudia Mwumbaji

  Wajibu wa kumsujudia Mwumbaji unatokana na ukweli kwamba yeye ni Mwumbaji. “Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba.” Soma pia Zaburi 96:5; Zaburi 100:3, Isaya 40:25, 26; Isaya 45:18.TK 272.2

  Katika Ufunuo 14 watu wanatakiwa kumsujudia Mwumbaji na kuzishika amri za Mungu. Moja kati ya amri hizi inamwelezea Mungu kuwa ni Mwumbaji: “Lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Kutoka 20:10, 11. Bwana anasema, Sabato ni “ishara ... mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.” Ezekieli 20:20.TK 272.3

  Kama Sabato ingeshikwa ulimwenguni kote, mwanadamu angeelekezwa kwa Mwumbaji kama mlengwa wa ibada. Kusingekuwa na mtu anayeabudu sanamu, asiyeamini kuwa hakuna Mungu, au mpagani. Kushika Sabato ni ishara ya utii kwake “aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.” Ujumbe unaoagiza wanadamu kumsujudia Mungu na kuzishika amri zake utawataka hasa kuishika amri ya nne.TK 272.4

  Tofauti na wale wanaozishika amri za Mungu na imani ya Yesu, malaika wa tatu anaelezea kundi lingine: “Mtu awaye yote akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake, au katika mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu.” Ufunuo 14:9, 10. Vinavyowakilishwa na mnyama, sanamu na alama ni vitu gani?TK 272.5

  Unabii ulio na vielelezo hivyo unaanzia katika Ufunuo 12. Joka aliyekuwa anataka kumwangamiza Kristo wakati wa kuzaliwa kwake anatajwa kuwa ni Shetani (Ufunuo 12:9); alimchochea Herode kumwua Mwokozi. Lakini wakala wa Shetani katika vita dhidi ya Kristo na watu wake katika kame za mwanzo ilikuwa dola ya Kirumi, ambako upagani ulikuwa ndiyo dini iliyo shamiri. Kwa hiyo, kwa maana nyingine joka ni kielelezo cha Rumi.TK 273.1

  Katika Ufunuo 13 kuna mnyama mwingine, “mfano wa chui,” ambaye joka alimpa “nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.” Kama vile Waprotestanti wengi wamekuwa wakiamini, kielelezo hiki kinawakilisha mamlaka ya Papa, ambayo ilipokea nguvu na kiti na mamlaka ambayo yalikuwa yanashikiliwa na dola ya Kirumi. Mnyama anayefanana na chui anazungumziwa hivi: “Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru ... Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni. Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.” Ufunuo 13:2, 5-7. Unabii huu unaofanana sana na maelezo ya pembe ndogo ya Danieli 7, bila shaka unaelezea mamlaka ya Papa.TK 273.2

  “Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.”—ile miaka mitatu na nusu, au siku 1260 za Danieli 7—ambapo mamlaka ya Papa iliwakandamiza watu wa Mungu. Kipindi hiki kilianza mwaka 538 B. K. na kumalizika mwaka 1798. Wakati huo mamlaka ya Papa ilipata “jeraha la mauti,” na utabiri usemao “Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa,” (Ufunuo 13:10) ukawa umetimia.TK 273.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents