Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Shetani Ameshindwa

  Kama walio ndotoni, waovu watatazama kutawazwa kwa Mwana wa Mungu. Wataona mikononi mwake mbao za sheria ya mbinguni waliyoipuuza. Watashuhudia sauti kubwa ya kutukuza kutoka kwa waliookolewa, na wimbi la sauti linapopaa juu ya makutano hadi kufika nje ya jiji, wote watasema, “Ni makuu, na ya ajabu, matendo yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi.” Ufunuo 15:3. Wataanguka kifudifudi, wakimwabudu Mfalme wa uzima.TK 400.4

  Shetani ataonekana kupooza. Yeye aliyekuwa kerubi afunikaye, sasa atakumbuka pale alipoanguka. Kutoka kwenye halmashauri ambapo alikuwa anaheshimiwa sasa ameondolewa milele. Atamwona mwingine sasa akisimama karibu na Baba, malaika mwenye enzi. Atajua kwamba nafasi hii ya kutukuka ya malaika huyu ingekuwa yake..TK 400.5

  Kumbukumbu zitamjia za hapa ambapo palikuwa nyumbani akiwa hana hatia, , amani na ridhaa alivyokuwa navyo mpaka wakati wa uasi wake. Atakumbuka kazi aliyoifanya kati ya wanadamu na matokeo yake, audui wa mwanadamu kwa mwanadamu mwenzake, uharibifu mbaya wa maisha, mapinduzi ya watawala, machafiiko, migogoro, na mapinduzi. Atakumbuka jitihada zake ambazo hazikukoma katika kuipinga kazi ya Kristo. Atapoangalia matunda ya kazi yake ataona kushindwa tu. Tena na tena katika pambano kuu amekuwa akishindwa na kulazimika kukubali..TK 401.1

  Kusudi la mwasi mkuu daima limekuwa ni kuthibitisha kwamba serikali ya mbinguni inawajibika kwa uasi. Amewaongoza makutano wengi kukubali maelezo yake. Kwa miaka mingi kiongozi huyu wa udanganyifu amebadilisha ukweli kwa kuweka uongo. Lakini sasa muda utakuwa umefika ambapo historia na tabia ya Shetani itafichuliwa. Katika jitihada zake za mwisho za kumpindua Kristo, kuwaangamiza watu wake na kuutwaa mji wa Mungu, mdanganyifu mkuu amefunuliwa kikamilifu. Wale walioungana naye wataona kushindwa kabisa kwa makusudi yake.TK 401.2

  Shetani ataona kuwa kuasi kwake kwa hiari kumemfanya asifae kuwa mbinguni. Amezizoeza nguvu zake kufanya vita dhidi ya Mungu. Sasa usafi na upatanifu uliopo mbinguni kwake ungekuwa ni mateso. Atasujudu na kukiri haki ya hukumu yake.TK 401.3

  Kila swali la ukweli na makosa katika pambano la muda mrefu sasa litakuwa limewekwa wazi. Matokeo ya kuweka pembeni utaratibu wa mbinguni yatakuwa yamewekwa wazi na kuonekana kwa ulimwengu wote. Historia ya dhambi itakuwepo milele zote kama ushahidi kwamba uwepo wa sheria ya Mungu umefungamana na furaha ya viumbe wote aliowaumba. Ulimwengu wote, wale walio waaminifu na waasi kwa sauti moja watasema, “Ni za haki, na za kweli, njia zako, Ee Mfalme wa watakatifu”TK 401.4

  Saa itakuwa imefika ambapo Kristo atatukuzwa juu ya kila jina linalojulikana. Kwa sababu furaha iliyokuwa mbele yake-ili kwamba awalete wana wengi kwenye utukufu-aliuvumilia msalaba, atawaangalia waliokombolewa, wakiwa wamefanywa upya katika sura yake. Ataona ndani yao matokeo ya maumivu yake, na ataridhika. Isaya 53:11. Kwa sauti itakayowafikia makutano wenye haki na waovu atasema: “Tazama gharama ya damu yangu, kwa ajili ya hawa niliteseka, kwa ajili ya hawa nilikufa.”TK 401.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents