Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mlandano wa Kuvutia

  Wakati ambapo kwenye ujio wa kwanza Wakristo Wayahudi, kwa siri, walikuwa wanaikanyaga sheria ya Mungu; kwa nje waliyashika matakwa yake kwa ushupavu, wakiijaza mahitaji yanayotaka umakini zaidi na kufanya utii kuwa mzigo mzito kuubeba. Kwa namna ile ile ambavyo Wayahudi walijidai kuiheshimu sheria; ndivyo Wakatoliki wanavyodai kuuheshimu msalaba.TK 345.3

  Wanaweka misalaba juu ya makanisa, madhabahu, na mavazi yao. Kila mahali nembo ya msalaba, kwa nje, inapewa heshima na kuinuliwa. Lakini mafundisho ya Kristo yamezikwa chini ya mapokeo yasiyo na mantiki na misimamo mikali kwenye mambo madogo. Watu waaminifu wamewekwa katika hofu ya ghadhabu ya Mungu aliyekasirishwa, wakati ambapo watu wenye vyeo ndani ya kanisa wanaishi maisha ya anasa na kujifurahisha kwa tamaa.TK 345.4

  Ni jitihada za kudumu za Shetani kuipotosha tabia ya Mungu, asili ya dhambi, na mambo ya kufa na kupona ndani ya pambano kuu. Udanganyifu wake unawapa wanadamu uhalali wa kutenda dhambi. Wakati huo huo yanawafanya watunze dhana za uwongo juu ya Mungu ili wamheshimu kwa hofu na chuki badala ya upendo. Kwa njia ya dhana zilizopotoshwa juu ya tabia za Mungu, mataifa ya kipagani yalikuwa yanaongozwa kuamini kuwa kafara za binadamu zilikuwa za lazima ili kupata kibali kutoka kwa miungu. Ukatili wa kutisha ulikuwa unafanyika isivyo halali chini ya mitindo kadhaa ya ibada ya sanamu.TK 346.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents