Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Siyo Mapenzi ya Mungu

  Haukuwa mpango wa Mungu kwamba Waisraeli wazunguke jangwani kwa miaka arobaini; alitamani kuwaongoza moja kwa moja hadi Kanaani na kuwafanya taifa takatifu, watu wenye furaha. Lakini, “hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.” Waebrania 3:19. Kwa namna hiyo hiyo, hayakuwa mapenzi ya Mungu kwamba kuja kwa Kristo kuchelewe na watu wake wakae kwa miaka mingi katika ulimwengu huu wa dhambi na huzuni. Kutokuamini kuliwatenganisha na Mungu. Ni kwa sababu ya rehema kwa ulimwengu, Yesu anakawia kuja ili wenye dhambi wasikie onyo na kutafuta kimbilio kabla ya kumwagwa kwa ghadhabu ya Mungu.TK 284.1

  Wakati huu, kama ilivyokuwa nyakati za zamani, kuuhubiri ukweli kutachochea upinzani. Wengi wakiwa na kijicho watashambulia tabia na nia za wale wanaosimama kuutetea ukweli usiopendwa. Eliya aliambiwa kuwa ni mtaabishaji wa Israeli, Yeremia aliitwa msaliti, na Paulo mwenye kulinajisi hekalu. Tangu siku zile hadi sasa, wale ambao ni waaminifu kwenye ukweli wamekuwa wakishutumiwa kuwa ni wachochezi, waasi, na wenye kuleta mafarakano.TK 284.2

  Maungamo ya imani yaliyofanywa na watakatifu na wafla dini, vile vielelezo vya utakatifu na uadilifu usiobadilika, huamsha ujasiri kwa wale ambao sasa wanaitwa kusimama kama mashahidi wa Mungu. Kwa mtumishi wa Mungu kwa wakati huu amri inasema, “Piga kelele, usiache, paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.” “Nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu.” Isaya 58:1; Ezekieli 33:7.TK 284.3

  Kipingamizi kikubwa cha ukweli kukubalika ni usumbufu na shutuma zinazoambatana nao. Hii ndiyo hoja pekee dhidi ya ukweli ambayo watetezi wake hawakuweza kuishinda. Lakini wafuasi wa kweli Wakristo hawasubiri hadi ukweli upendwe na watu wengi. Wanaukubali msalaba, pamoja na Paulo wakihesabu kuwa, “dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana”; pamoja yule wa zamani aliyekuwa, “akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri.” 2 Wakorintho 4:17; Waebrania 11:26.TK 284.4

  Inatupasakuuchagua ukweli kwa sababu ni ukweli na kumwachia Mungu matokeo yote. Watu wanaofuata kanuni, wenye imani, na wanaothubutu wana wajibu juu ya matengenezo katika ulimwengu. Kupitia watu hawa kazi ya matengenezo kwa wakati huu ni lazima isukumwe mbele.TK 285.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents