Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kifungo Cha Shetani

  Tukio linalotokea sasa lilitabiriwa katika huduma yenye taadhima ya Siku ya Upatanisho. Wakati dhambi za Israeli zilipokuwa zimekwisha kuondolewa kutoka katika hema kwa njia ya damu ya kafara ya dhambi, mbuzi wa Azazeli aliletwa akiwa hai mbele za Bwana. Kuhani mkuu aliungama juu yake “uovu wote wa wana wa Israeli, . . . akiziweka “juu ya kichwa chake yule mbuzi” Mambo ya Walawi 16:21. Kwa namna hiyo hiyo wakati kazi ya upatanisho katika hekalu la mbinguni itakapokamilika, ndipo, katika mbele za Mungu na malaika wa mbinguni na jeshi la waliokombolewa, dhambi za watu wa Mungu zitawekwa juu ya Shetani; atahukumiwa kuwa na hatia ya uovu wote aliosababisha wakautenda. Kama vile mbuzi wa Azazeli alivyopelekwa katika nchi isiyokaliwa na watu, ndivyo Shetani atakavyondolewa hadi kwenye dunia iliyo ukiwa.TK 393.2

  Baada ya kuelezea matukio ya kuja kwa Bwana, mwandishi wa Ufunuo anaendelea: “Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.” Ufunuo 20:1-3.TK 393.3

  “Kuzimu” kunawakilisha dunia ikiwa katika hali ya giza na kuchanganyikiwa. Akiitazamia siku ile kuu ya Bwana Yeremia anasema: “Naliiangalia nchi, na tazama, ilikuwa ukiwa, haina watu; naliziangalia mbingu, nazo zilikuwa hazina nuru. Naliiangalia milima, na tazama, ilitetemeka, na milima yote ilisogea huko na huko. Nikaangalia, na tazama, hapakuwa na mtu hata mmoja, na ndege wote wa angani wamekwenda zao. Nikaangalia, na tazama, shamba lililozaa sana limekuwa ukiwa, na miji yake yote ilikuwa imebomoka.” Yeremia 4:23- 26.TK 393.4

  Hapo patakuwa makao ya Shetani na malaika zake waovu kwa miaka 1,000. Akiwa amezuiliwa duniani, hataweza kuufikia ulimwengu mwingine kuwajaribu na kuwasumbua wale ambao hawajaanguka. Kwa maana hiyo “amefungwa.” Hakuna atakayesalia ambaye kwake Shetani ataonesha uwezo wake. Atakuwa ameondolewa kutoka katika kazi ya udanganyifu na maangamizi ambayo ilikuwa furaha yake pekee.TK 394.1

  Isaya, akiutazama wakati wa Shetani kutupwa chini, alisema kwa mshangao: “Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifaLNawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu. Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme; Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?’ Isaya 14:12-17.TK 394.2

  Kwa miaka 6000 gereza la Shetani liliwapokea watu wa Mungu, lakini Kristo atavivunja vifungo vyake na kuwaweka wafungwa huru. Yeye peke yake na akiwa na malaika zake waovu atapata madhara ya dhambi: “Wafalme wote wa mataifa wamezikwa wote kwa heshima, Kila mmoja ndani ya nyumba yake mwenyewe (kaburi). Bali wewe umetupwa mbali na kaburi lako, Kama chipukizi lililochukiza kabisa; Hutaungamanishwa pamoja nao katika mazishi, Kwa maana umeiharibu nchi yako, umewaua watu wako.”Isaya 14:18-20.TK 394.3

  Kwa miaka 1,000, Shetani atayaona matokeo ya uasi wake dhidi ya sheria ya Mungu. Mateso yake yatakuwa makali. Sasa atakuwa ameachwa ili atafakari juu ya kazi aliyoifanya tangu alipoasi na kuisubiri hatima yake ya kutisha wakati atakapolazimika kuadhibiwa.TK 394.4

  Wakati wa miaka 1,000 kati ya ufufuo wa kwanza na wa pili, hukumu ya waovu itafanyika. Paulo analionesha hili kuwa ni tukio litakalofuatia ujio wa pili. lWakorintho 4:5. Wenye haki watatawala kama wafalme na makuhani. Yohana anasema: “Kisha nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; . . . Watakuwa makuhani wa Mungu na Wakristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.” Ufunuo 20:4-6.TK 395.1

  Wakati huo “watakatifu watauhukumu ulimwengu” lWakorintho 6:2. Kwa kuungana na Kristo watawahukumu waovu, wakiliamua kila shauri sawasawa na matendo yaliyofanyika katika mwili. Kisha kiwango ambacho waovu wanapaswa kuteseka kitapimwa, sawasawa na matendo yao na kuandikwa mbele ya majina yao katika kitabu cha mauti.TK 395.2

  Shetani na malaika waovu watahukumiwa na Kristo na watu wake. Paulo anasema: “Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu?” lWakorintho 6:3. Yuda anasema: “Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.” Yuda 6.TK 395.3

  Mwisho wa miaka 1,000 ufufuo wa pili utafanyika. Kisha waovu watafufuliwa kutoka katika wafu na kuja mbele za Mungu ili kufanyiwa “hukumu iliyoandikwa.” Zaburi 149:9. Kwa hiyo mwandishi wa ufunuo anasema: “Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.” Ufunuo 20:5. Na Isaya, kuhusu waovu anasema: “nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.” Isaya 24:22.TK 395.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents