Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Luther Ashitakiwa kwa Uasi wa Kidini

  Aleander akitumia ujuzi na lugha ya ushawishi alijiweka katika nafasi ya kumpindua Luther kama adui wa kanisa na wa serikali. Alisema, “Katika makosa ya Luther kuna mambo ya kutosha” kumfanya achomwe sawa na “mamia ya maelfu ya waasi.”TK 95.2

  “Wafuasi wote hawa wa Luther ni nini? Ni kundi la walimu wenye dharau, mapadre wasio na maadili, watawa wa kiume waliopotoka, wanasheria wajinga, na wakuu walioporomoka kimaadili... Wakatoliki ni bora kiasi gani katika idadi, uwezo na nguvu, ukiwalinganisha na hawa wafuasi wa Luther! Amri ya pamoja kutoka kwenye mkutano huu maarufu itawaelimisha watu wa kawaida, itawaonya wajinga, wanaoyumbayumba kufanya maamuzi, na itatoa nguvu kwa wadhaifu.” 67Ibid., ch. 3.TK 95.3

  Hoja za namna hii bado hutolewa dhidi ya wote wanaothubutu kuyaleta mafundisho ya Neno la Mungu kwa uwazi. “Hawa wahubiri wa mafundisho mapya ni akina nani? Hawana elimu, ni wachache kwa idadi, na wanatoka kwenye daraja la maskini. Na bado wanadai kuwa wanao ukweli, na kwamba ndio walioteuliwa na Mungu. Ni wajinga na wamedanganyika. Ni ubora wa juu jinsi gani unaodhihirishwa na kanisa letu kwa idadi ya watu na mvuto!” Hoja hizi haziondoi tena mashaka sasa kuliko ilivyokuwa nyakati za wanamatengenezo.TK 95.4

  Luther hakuwepo ili kuushinda utetezi wa utawala wa Papa kwa ukweli wa Neno la Mungu ulio wazi na wenye kushawishi. Kulikuwepo na mwelekeo wa jumla siyo tu wa kumhukumu Luther na mafundisho aliyofundisha, bali kama ingewezekana kuung’oa uasi. Yale yote ambayo Kanisa la Roma lingeweza kuyasema kwa ajili ya uthibitisho wake yalikuwa yamesemwa. Tangu wakati huo tofauti kati ya ukweli na uongo ilikuwa inaonekana dhahiri kwa kadiri pambano lilivyokuwa wazi.TK 96.1

  Sasa Bwana alimsukuma mmoja wa wajumbe wa mkutano kufafanua undani wa madhara ya udhalimu wa utawala wa Papa. George, Mtawala wa jimbo la Saksoni, alisimama mbele ya lile kusanyiko la kifalme akachambua kwa usahihi wa ajabu udanganyifu na machukizo ya utawala wa Papa:TK 96.2

  “Vilio vya dhuluma vinasikika kwenye Kanisa la Roma. Aibu yote imewekwa kando, na lengo lao pekee ni...pesa, pesa, pesa,...kiasi kwamba wahubiri waliokuwa wanatakiwa kufundisha ukweli, hawatamki chochote isipokuwa uongo, na siyo tu wanavumiliwa, bali pia wanatuzwa, kwa sababu, kwa kadiri uongo unavyokuwa mkubwa ndiyo faida inavyozidi kuwa kubwa kwao. Kutoka kwenye chemchemi hii mbovu ndipo yanapotoka maji haya machafu. Uuaji na ulafi wa mali vinashikamana... Ni huzuni, kashfa iliyosababishwa na makasisi inazitupa roho nyingi maskini kwenye hukumu ya milele. Matengenezo ya jumla ni lazima yafanyike.” 68Ibid., ch. 4. Ukweli kuwa mzungumzaji alikuwa adui mkubwa wa Mwanamatengenezo, ulisababisha mvuto mkubwa kwa maneno yake.TK 96.3

  Malaika wa Mungu waliliangazia nuru giza la uongo na kuifunua mioyo kwenye ukweli. Uwezo wa Mungu wa ukweli uliwadhibiti hata maadui wa matengenezo na ulitayarisha njia kwa ajili ya kazi kubwa iliyokuwa karibu kufanyika. Sauti ya Aliye mkuu kuliko Luther ilikuwa imesikika katika kusanyiko lile.TK 96.4

  Iliteuliwa kamati ya kuandaa orodha ya dhuluma za utawala wa Papa ambazo zilikuwa mzigo mzito kwa watu wa Ujerumani. Orodha hiyo iliwasilishwa kwa mfalme, ikiwa na madai ya kumtaka achukue hatua za kuziondoa dhuluma hizo. Walalamikaji walisema, “Ni jukumu letu kuzuia uangamivu na kuvunjiwa heshima watu wetu. Kwa sababu hiyo kwa unyenyekevu mkuu na kwa umuhimu mkubwa tunakutaka uamuru matengenezo ya jumla, na kuhakikisha yanakamilika.” 69Ibid.TK 97.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents