Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ufunuo Wadhihirika kwa Bengel

    Katika Ujerumani fundisho hili lilikuwa limefundishwa na Bengel, mchungaji wa Kilutheri na mwanazuoni wa Biblia. Wakati akiandaa mahubiri yake kutoka Ufunuo 21, nuru ya ujio Wakristo ilikuja katika akili zake. Unabii wa Ufunuo ulidhihirika katika akili zake. Kwa kuwa alijawa na fikra juu ya umuhimu na utukufu wa matukio yaliyoelezewa na nabii aliyeandika kitabu cha Ufunuo, alilazimika kuliacha jambo hilo kwa muda. Alipokuwa madhabahuni lilimjia tena kwa udhahiri. Tangu wakati huo aliazimu kusoma unabii na muda si mrefu aliamini kuwa ujio wa Yesu ulikuwa umekaribia. Tarehe aliyoiweka ya ujio wa pili ilikuwa ndani ya miaka michache kutoka ile iliyowekwa na Miller.TK 231.1

    Maandishi ya Bengel yalienea katika jimbo lake la Wiirtemberg na sehemu nyingine za Ujerumani. Ujumbe wa kurudi kwa Kristo ulisikika Ujerumani wakati ule ule ulipokuwa unavuta usikivu wa wengi katika nchi nyingine.TK 231.2

    Kule Geneva, Gaussen alihubiri ujio Wakristo. Alipojiunga na kazi ya uchungaji alikuwa na mwelekeo wa mashaka. Katika ujana wake alikuwa anatamani kujifunza unabii. Baada ya kusoma kitabu cha Rollin kiitwacho “Ancient History,” akili yake ilivutiwa na sura ya pili ya kitabu cha Danieli. Alishangazwa sana na usahihi ambao unabii huo ulikuwa umetimia. Hapa kulikuwa na ushahidi wa uvuvio wa Maandiko. Hakuridhika na maelezo ya udhuru na katika kusoma Biblia alielekezwa kwenye imani chanyaTK 231.3

    Aliamini kuwa ujio Wakristo ulikuwa karibu. Kwa kuwa alivutiwa na umuhimu wa ukweli, alitamani kuuflkisha kwa watu. Lakini imani ya wengi kwamba unabii wa Danieli hauwezi kueleweka ilikuwa kikwazo kikubwa. Hatimaye aliazimu—kama alivyofanya Farel kabla yake katika kueneza Injili kule Geneva—kuanza na watoto, ambao alitarajia wangewavuta wazazi. Alisema, “Nikakusanya hadhira ya watoto... kundi linapokuwa kubwa, inapoonekana kwamba wanasikiliza, wanapendezwa, wanavutiwa, kwamba wanaelewa na kuielezea mada husika, bila shaka nitakuwa na kundi lingine muda si mrefu, na kwa upande wao, watu wazima wataona kuwa kuna haja ya kukaa na kujifunza. Jambo hilo likifanyika lengo litakuwa limetimia. 214L. Gaussen, Daniel the Prophet, vol. 2, dibaji.TK 231.4

    Alipokuwa anahutubia watoto, watu wazima walikuja kusikiliza. Njia zote katika kanisa lake zilijaa wasikilizaji, watu wenye vyeo na wasomi, wageni na watu wa mataifa mengine waliokuwa wanatembelea Geneva. Kwa njia hiyo ujumbe ulikwenda sehemu zingine.TK 232.1

    Kwa kuwa alitiwa moyo, Gaussen alichapisha masomo yake akitumaini kuinua usomaji wa vitabu vya unabii. Baadaye alikuwa mwalimu katika chuo cha teolojia, na Jumapili aliendelea na kazi yake ya ukatekista, akiwahutubia watoto na kuwafundisha Maandiko. Kutoka katika kiti chake cha uprofesa, hadi katika kiwanda cha kuchapa vitabu na kufundisha watoto, kwa miaka mingi alichangia sana katika kuwafanya watu wengi wasome unabii uliokuwa unaonesha kuwa ujio wa Bwana ulikuwa umekaribia.TK 232.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents