Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushawishi kwa Wanaopenda Anasa

    Kwa wasiojizuia nafsi, wanaopenda anasa, wenye tamaa ya mwili, imani ya mizimu inaleta mitego isiyo na ustadi mkubwa. Katika hali zake za kawaida wanatafuta kile kinachopatana na mielekeo yao. Shetani anaziwekea alama dhambi ambazo kila mwanadamu huelekea kuzitenda na kisha anahakikisha kuwa fursa hazitakosekana ili kuyatukuza mazoea. Anawajaribu wanadamu kupitia kutokuwa na kiasi ili kudhoofisha uwezo wa kimwili, kiakili, na kimaadili. Anawaangamiza watu wengi kupitia uendekezaji wa tamaa, na kuukatili mwili. Ili kukamilisha kazi yake, roho wanatamka kuwa “elimu ya kweli inamweka mwanadamu juu ya sheria yote”; kwamba “chochote kilichopo, ni sahihi” kwamba “Mungu hahukumu”; na kwamba “dhambi zote...si hatia.” Wakati watu wanapoamini kuwa tamaa ndiyo kanuni ya juu zaidi, kwamba uhuru ni kibali cha mtu kufanya kile atakacho, kwamba mwanadamu anawajibika kwake mwenyewe tu, ni nani atakayeshangaa kuona uovu unafurika kila mahali? Watu wengi kwa uchu wanakubali vishawishi vya tamaa. Shetani anawanasa kwenye wavu wake wengi wa wale wanaokiri kumfuata Kristo.TK 339.1

    Lakini Mungu ametoa nuru ya kutosha kugundua mitego. Msingi halisi wa imani ya mizimu unapingana na Maandiko. Biblia inatamka kuwa wafu hawajui neno lolote, kwamba mawazo yao yametoweka; hawana sehemu katika furaha ama huzuni za walio hai.TK 339.2

    Zaidi ya hayo, Mungu amekataza mawasiliano ya udanganyifu na roho zilizoanguka. Hizi “roho mashuhuri” kama walivyoitwa hawa wageni kutoka ulimwengu mwingine, wametamkwa na Biblia kuwa ni “roho za maShetani.” Angalia Hesabu 25:1-3; Zaburi 106:28; lWakorintho 10:20; Ufunuo 16:14. Ilikatazwa kuhusiana nao, adhabu ya kifo ilitolewa kwa wasiotii Walawi 19:31; 20:27. Lakini imani ya mizimu imeingia kwenye fani ya sayansi, imevamia makanisa, na inakubalika kwenye vyombo vya kutunga sheria, na hata ndani ya nyumba za wafalme. Udanganyifu huu mkubwa ni mbinu ya kuamsha kwa mbinu mapya za uchawi uliokuwa umeshutumiwa zamani.TK 339.3

    Kwa kudai kuwa wanadamu waovu wapo mbinguni, Shetani anauambia ulimwengu kuwa, “Haijalishi kama unamwamini au humwamini Mungu na Biblia, ishi upendavyo; mbinguni ni nyumba yako” Neno la Mungu linasema: “Ole wao wasemao kwamba uovu ni wema, na kwamba wema ni uovu; watiao giza badala ya nuru, na nuru badala ya giza” Isaya 5:20.TK 340.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents