Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Utakaso ni Nini?

  Nadharia zenye makosa za utakaso zinatokana pia na kuiacha sheria ya Mungu. Nadharia hizi ambazo, zina mafundisho ya uongo na matokeo hatari ya utendaji wake, kwa ujumla ndizo zinazopendwa.TK 290.2

  Paulo anatangaza: “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu.” Biblia kwa uwazi inafundisha maana ya utakaso na namna ya kuupata. Mwokozi aliwaombea wanafunzi wake: “Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.” Na Paulo anafundisha kwamba wauamini wanatakiwa, “kutakaswa na Roho Mtakatifu.” 1 Wathesalonike 4:3; Yohana 17:17; Warumi 15:16.TK 290.3

  Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote.” Yohana 16:13. Na mtunga Zaburi anasema: “sheria yako ndiyo kweli” Kwa sababu, “sheria ya Mungu ni takatifu na ya haki na njema” tabia itakayojengwa kwa njia ya utii wa sheria hiyo itakuwa takatifu. Kristo ni kielelezo kamili cha tabia hiyo. Anasema nimezishika “amri za Baba yangu” “Nafanya siku zote yale yampendezayo.” Yohana 15:10; 8:29. Inawapasa wafuasi Wakristo wawe kama Yeye - kwa neema ya Mungu watengeneze tabia zinazopatana na kanuni za sheria yake takatifu. Huu ndio utakaso wa Biblia.TK 290.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents