Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ujasiri wa Berquin

  Ari ya Berquin ilikuwa inaendelea kuwa thabiti. Alidhamiria kuchukua hatua za ushupavu zaidi. Hatasimama tu kutetea ukweli, atakuwa anashambulia upotovu. Wapinzani wake wenye nguvu walikuwa ni watawa wasomi wa idara ya teolojia katika Chuo Kikuu cha Paris, moja ya mamlaka ya juu sana ya kidini katika taifa. Kutoka kwenye maandishi ya madaktari hawa, Berquin alipata mapendekezo kumi na mawili aliyoyatangaza hadharani kuwa “yalikuwa yanapingana na Biblia,” na alimwomba mfalme awe mwamuzi kwenye ubishani huo.TK 139.2

  Kwa furaha na kutaka kunyenyekesha kujikweza kwa watawa hawa, aliwaalika wafuasi wa Kanisa la Roma kukitetea kile wanachokiamini kupitia Biblia. Silaha hii ingewafaa kidogo sana; mateso na nguzo ya kuchomea watu moto vilikuwa ni silaha walizofahamu vizuri namna ya kuzitumia. Walijikuta karibu na kutumbukia kwenye shimo walilotaka kumtupia Berquin. Walitafuta namna ya kutoroka.TK 139.3

  “Ni wakati ule sanamu ya bikira iliyokuwa katika moja ya kona za mtaa mmoja ilipoharibiwa.” Makundi ya watu yalimiminika kwenda kwenye eneo hilo kwa hasira na maombolezo. Mfalme aliguswa sana na jambo hilo. “Haya ni matunda ya mafundisho ya Berquin,” walilalamika watawa. Kila kitu kinaelekea kupinduliwa kwa njama za hawa Walutheri -dini, sheria, na ufalme wenyewe.” 134Ibid.TK 139.4

  Mfalme aliondoka Paris, na watawa waliachwa huru kutenda wapendavyo. Berquin alishtakiwa na kuhukumiwa kifo, na ili Francis asiingilie kumwokoa, hukumu ilitekelezwa siku hiyo hiyo iliyokuwa imepitishwa. Mchana, mkutano mkubwa ulikusanyika kushuhudia tukio hilo, na wengi waliliangalia tukio hili kwa mshangao mkubwa kwa kuwa mhanga wa tukio hili alikuwa amechaguliwa toka kati ya watu bora na jasiri kabisa miongoni mwa familia za watu waungwana nchini Ufaransa. Mshangao, uchungu, kubeza, na chuki zilionekana kwenye nyuso zilizokuwa na simanzi kwa watu waliokuwa wanaongezeka, na juu ya uso wa mtu mmoja peke yake hakukuwa na dalili yoyote ya majonzi. Mfia dini huyo alikuwa anahisi uwepo wa Bwana wake.TK 140.1

  Uso wa Berquin ulikuwa unang’aa kwa nuru ya mbinguni. Alikuwa amevaa “vazi lenye manyoya, jaketi la kubana la hariri, kitambaa chenye urembo na vazi la kubana la rangi ya njano lililofunika toka miguuni.” 135D’Aubigne, History of the Reformation in Europe in the Time of Calvin, bk 2, ch. 16. Alikuwa tayari kushuhudia imani yake mbele ya Mfalme wa wafalme na haikupaswa kuwepo dalili yoyote ya maombolezo kama kisingizio kwa furaha yake.TK 140.2

  Kadri msafara ulivyokwenda taratibu kupitia mitaa iliyokuwa imejaa watu, watu walishangazwa na mwonekano wa ushindi mkubwa na wenye furaha aliokuwa nao. Walisema, “Anafanana na mtu yule anayekaa hekaluni, ambaye hutafakari kuhusu mambo matakatifu.”TK 140.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents