Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Makusudi ya Siri

    Kuna kumbukumbu pia kwa ajili ya dhambi za wanadamu. “Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.” “Kila neno lisilo maana, watakalolinena wanadamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.” “Kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa.” Mambo ya siri yanaonekana kwenye kitabu, kwani Mungu “atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo” Mhubiri 12:14; Mathayo 12:36, 37; 1 Wakorintho 4:5. Mbele ya kila jina kwenye vitabu vya mbinguni limeandikwa kila neno lisilofaa, kila tendo la ubinafsi, kila wajibu usiotimizwa, na kila dhambi ya siri. Maonyo yaliyotumwa kutoka mbinguni au makaripio yaliyopuuzwa, wakati uliopotea, mvuto uliowekwa kwa mema au kwa mabaya pamoja na matokeo yake ya mwisho, yote yanaandikwa na malaika anayetunza kumbukumbu.TK 297.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents