Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mnyama Mwenye Pembe kama za Mwanakondoo

  Unabii wa Ufunuo 13 unatangaza kwamba mnyama mwenye pembe kama za Mwanakondoo “Aifanya dunia na wote wakaao ndani yake” kuuabudu utawala wa Papa-ambao umewakilishwa na mnyama “mfano wa chui” Mnyama mwenye pembe mbili atawaambia “wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama.” Zaidi ya hayo atawalazimisha wote “...wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa” watiwe chapa ya mnyama. Ufunuo 13:11-16. Marekani ndiyo mamlaka inayowakilishwa na mnyama mwenye pembe kama za Mwanakondoo. Unabii huu utatimizwa wakati Marekani itakapolazimisha kushika Jumapili, ambayo Roma inadai ni kuukiri ukuu wake.TK 351.1

  “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote, ikamstaajabia mnyama yule.” Ufunuo 13:3. Jeraha la mauti linatuonesha kwenye anguko la utawala wa Papa mwaka 1798. Baada ya hayo anasema nabii, “jeraha lake la mauti likapona: Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.” Paulo anasema kuwa “mtu wa kuasi” atafanya kazi yake ya udanganyifu karibu na mwisho wa wakati. 2Wathesalonike 2:3-8. Na “watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima” Ufunuo 13:8. Katika ulimwengu wa zamani na wa sasa utawala wa Papa utapokea heshima inayotolewa kwa adhama ya Jumapili.TK 351.2

  Tangu katikati ya kame ya kumi na tisa, wanafunzi wa unabii waliuleta ushuhuda huu katika ulimwengu. Na sasa tunaona kasi ya maendeleo katika kutimia kwa utabiri huu. Miongoni mwa walimu wa Kiprotestanti lipo dai lile lile la kuwepo mamlaka kutoka mbinguni juu ya kuishka Jumapili, na bado uthibitisho wa Maandiko unakosekana, kama ilivyo kwa viongozi wa utawala wa Papa. Madai kwamba hukumu za Mungu zitawakalia wanadamu kwa uvunjaji wa sabato ya jumapili yatarudiwa; na tayari hoja zimeanza kutolewa.TK 351.3

  Kanisa la Roma lina werevu wa ajabu. Lina uwezo wa kufahamu kabla, nini kitatokea baadaye - kwamba makanisa ya Kiprotestanti yanalipatia heshima kuu kwa kuikubali sabato ya uongo na kwamba wanajiandaa kuilazimisha kwa njia ambayo lilikuwa linaitumia zamani. Litakuwa tayari kiasi gani kuwasaidia Waprotestanti katika kazi hii, si vigumu kubashiri!TK 351.4

  Kanisa Katoliki la Roma linaunda taasisi kubwa ambayo ipo chini ya udhibiti wa mamlaka ya Papa, wapo mamilioni ya waleta habari wake katika kila nchi wakifungwa kifungo cha utii kwa Papa, bila kujali wapo katika nchi au serikali gani. Ingawa wanaweza kuapa kuwa waaminifu kwa nchi waliyomo, lakini nyuma yake wana kiapo cha utii kwa Roma.TK 352.1

  Historia inao ushuhuda wa jitihada zisizokoma na zenye ustadi za kujipenyeza kwa Kanisa la Roma kwenye mambo ya mataifa, na likipata nafasi, litaitumia kufanikisha malengo yake hata kama ni kwa uangamivu wa watawala na watu. 240John Dowling, The History of Romanism, bk. Ch. 6, sec. 55; and Mosheim, bk. 3’ cent. 11, pt. 2, sec. 9, notel 7.TK 352.2

  Kanisa la Roma linajivuna kuwa halibadiliki. Waporotestanti wanafahamu kidogo juu ya kile wanachofanya wanapopendekeza kupata msaada kutoka kwenye Kanisa la Roma katika kazi ya kuiinua Jumapili. Wakiwa wamejielekeza katika kusudi lao, Kanisa la Roma linalenga katika kuijenga upya mamlaka yake, kuurejesha ukuu wake uliopotea. Hebu kanuni iwekwe tena kuwa kanisa linaweza kudhibiti mamlaka ya serikali; kwamba taratibu za kanisa zilazimishwe na sheria za nchi; kwa ufupi, kwamba mamlaka ya kanisa na ya nchi yatawale dhamiri - ndipo Kanisa la Roma litakuwa limejihakikishia ushindi wake.TK 352.3

  Ulimwengu wa Kiprotestanti utagundua makusudi ya Kanisa la Roma wakati utakapokuwa umechelewa kujinasua kwenye mtego. Kanisa la Roma kwa ukimya linakua kuelekea kwenye mamlaka. Mafundisho yake yana mvuto kwenye mabunge ya kutunga sheria, makanisani, na katika mioyo ya wanadamu. Linayaimarisha majeshi yake ili kuendeleza malengo yake muda utakapofika. Tamaa yake pekee ni kupata mazingira muafaka. Yeyote atakayeamini na kulitii Neno la Mungu ataambulia shutuma na mateso.TK 352.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents