Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hati ya Uhuru

    Tamko la uhuru wa Marekani linasema kuwa: “Tunaaminikuwa ukweli huu ni bayana; kwamba watu wote wameumbwa sawa; kwamba wamepewa na Mwumbaji wao haki kadhaa zisizoweza kuondolewa; kwamba miongoni mwa hizo ni uhai, uhuru, na kutafuta furaha.” Katiba inatoa uhakikisho wa heshima ya dhamiri: “Bunge halitatunga sheria yoyote inayohusu kuanzisha dini, au kupiga marufuku uhuru wa kufanya hivyo.”TK 191.1

    Walioiunda Katiba waliitambua kanuni ya milele kuwa uhusiano wa mwanadamu na Mungu, uko juu ya sheria zilizotungwa na wanadamu, na haki yake ya dhamiri haiondosheki...Ni kanuni anayozaliwa nayo ambayo hakuna kinachoweza kuing’oa.” 189Congressional Documents (U. S. A), serial No. 200, Document No. 271.TK 191.2

    Habari zilisambaa katika Ulaya yote kuhusu nchi ambayo kila mtu anaweza kufurahia matunda ya kazi yake na kuiridhisha dhamiri yake. Maelfu walifurika katika fukwe za Ulimwengu Mpya. Ndani ya miaka ishirini baada ya nanga ya kwanza kutiwa pale Plymouth (1620), maelfu wa Mahujaji walikuwa wamefanya makazi katika New England. “Hawakuomba chochote kutoka ardhini isipokuwa mapato ya haki ya kazi yao...Kwa ustahimilivu waliuvumilia upweke wa nyikani, wakiumwagilia mti wa uhuru kwa machozi yao, na kwa jasho la nyuso zao, hadi ulipokita mzizi chini ya nchi.”TK 191.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents