Kuhesabiwa Haki kwa Njia ya Imani
Fundisho kuu lililokuwa linafundishwa kwa uwazi zaidi na Luther la kuhesabiwa haki kwa njia ya imani, lilikuwa linaelekea kusahaulika kabisa; kanuni ya Kanisa la Roma la kutumainia matendo mema ili kuokolewa lilikuwa limechukua nafasi yake. Whitefield na wafuasi wa Wesley walikuwa waaminifu kutafuta kukubaliwa na Mungu. Hili walivyokuwa wamefundishwa, lilikuwa linapatikana kwa matendo mema na maagizo ya kidini.TK 164.4
Wakati Charles Wesley alipokuwa ameugua kiasi cha kuona kuwa kifo kilikuwa kinakaribia aliulizwa alipokuwa ameweka tumaini la uzima wa milele. Alijibu: “Nimetumia juhudi zangu wote kumtumikia Mungu.” Rafiki yake alionekana kutoridhishwa na jibu hili. Wesley alitafakari: “NiniL.Je, atazipora jitihada zangu? Sina kingine cha kutumainia.” Hilo lilikuwa giza lililokuwa limetanda katika kanisa, likiwageuza watu kutoka katika tumaini lao la pekee la wokovu-damu ya Mwokozi aliYesulubishwa.TK 165.1
Wesley na washirika wake walikuwa wameongozwa kuona kwamba sheria za Mungu huwa zinasambaa kwenye mawazo, maneno na matendo. Kwa juhudi na bidii kwenye maombi zina uwezo wa kushinda uovu wa moyo. Walikuwa wanaishi maisha ya kujikana nafsi na ya kujidhili, wakitunza kwa usahihi sana kila kipengele walichokuwa wanadhani kingewasaidia kupata utakatifu na kukubalika mbele za Mungu. Lakini jitihada zao zilikuwa bure kuwapatia uhuru kutoka kwenye laana ya dhambi ama kuzivunja nguvu zake.TK 165.2
Moto wa ukweli wa mbinguni, ambao tayari ulikuwa umezimika katika madhabahu za Uprotestanti, ulipasa kuwashwa upya kutoka kwenye mwenge wa kale wa Wakristo wa Bohemia. Baadhi ya wakimbizi hawa walipata hifadhi kule Saksoni, waliiendeleza imani ya kale. Wesley alipata nuru yake kutoka kwa Wakristo hawa.TK 165.3
John na Charles walitumwa kupeleka habari njema kule Amerika. Kwenye meli waliyokuwa wanasafiri nayo, lilikuwemo kundi la Wamoravia. Mawimbi makali yaliwasumbua, na John akiwa uso kwa uso na mauti, alijisikia kutokuwa na uhakika wa amani yake na Mungu. Wajerumani walidhihirisha utulivu na tumaini lililomshangaza sana. “Muda mrefu kabla nilikuwa nimeona umakini mkubwa katika mwenendo wao....Ilikuwa ni fursa ya kujaribiwa kwao kama walikuwa wamekombolewa kutoka kwenye roho ya hofu, kiburi, hasira na kisasi. Katikati ya wimbo walipokuwa wameanza huduma yao ya ibada, bahari ilichafuka na kulivunjavunja tanga na kuifunika kabisa meli na kumwaga maji yake katikati ya sitaha kana kwamba bahari tayari ilikuwa imetumeza. Sauti za kutisha za mayowe zilianza kusikika miongoni mwa Waingereza. Kwa utulivu kabisa Wajerumani walikuwa wanaendelea kuimba. Baadaye nilimuuliza mmoja wao, ‘Hamkuwa mmeogopa?’ Naye alinijibu, ‘Tunamshukuru Mungu maana hatukuwa tumeogopa.’ Nami nilimwuliza tena, ‘Lakini wanawake na watoto wenu nao hawakuwa wameogopa?’ Naye akajibu kwa upole, ‘Hapana, wanawake na watoto wetu hawaogopi kufa.’ “ TK 165.4