Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Katika Mji Mtakatifu.

  Kutoka katika jeshi la waliokombolewa, lisilo na idadi; kila jicho litaelekezwa kwa Yesu Kila jicho litauangalia utukufu wake yeye ambaye, “uso wake ulikuwa umeharibiwa sana zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu.” Isaya 52:14. Juu ya vichwa vya washindi Yesu ataweka taji za utukufii. Kwa kila mmoja kutakuwa na taji iliyo na “jina jipya” (Ufunuo 2:17) na maneno, “Mtakatifu kwa Bwana.” Katika kila mkono kutakuwa na mtende wa mshindi na kinubi king’aacho. Kisha malaika kiongozi anapopiga noti, kila mkono unavuta uzi kwa mguso wenye ujuzi katika fahari na sauti tamu yenye mvuto. Kila sauti inainuliwa kwa sifa za shukrani: “Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.” Ufunuo 1:5,6.TK 386.2

  Mbele ya mkutano mkubwa uliokombolewa kwa kafara kutakuwa na Mji Mtakatifu. Yesu atafungua malango, na mataifa ambao waliishika kweli wataingia ndani. Kisha sauti yake itasikika, “Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu.” Mathayo 25:34. Kristo atawasilisha kwa Baba yake wale aliowanunua kwa damu yake, Akisema: “mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.” “mimi naliwalinda kwa jina Iako ulilonipa” Waebrania 2:13;Yohana 17:12. Aha! Itakuwa ni saa ya ajabu ya kunyakuliwa wakati Baba wa milele, atakapowaangalia waliokombolewa kwa kafara ya Yesu, akiiona sura yake, madhara ya dhambi yakiwa yameondolewa, na kwa mara nyingine tena mwanadamu akiwa katika hali ya kupatanana Mungu.TK 386.3

  Furaha ya Mwokozi ni kuziona katika ufalme wa utukufu, roho ambazo zitakuwa zimekombolewa kutokana na matokeo ya uchungu na kudhalilishwa kwake. Waliokombolewa watashiriki furaha yake; watawaona wale waliokombolewa kwa maombi, kazi na kafara yao ya upendo. Mioyo yao itajazwa na furaha watakapoona mmoja amempata mwingine, na wale wengine kupata wengine zaidi.TK 387.1

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents