Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tumaini Kuu

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mpiga Mbiu wa Zama Mpya

  Mungu alikuwa ameliweka neno la ukweli ndani ya kinywa cha Wycliffe. Uhai wake ulilindwa na kazi zake ziliendelezwa hadi msingi ulipokuwa umewekwa kwa ajili Matengenezo. Wycliffe hakuunda mfumo wake wa matengenezo kutokana na yeyote aliyemtangulia. Yeye alikuwa mpiga mbiu wa zama mpya. Licha ya hivyo, katika ukweli aliouwasilisha kulikuwa na umoja na ukamilifu ambao wanamatengenezo waliofuatia hawakuweza kuupita na pia ambao baadhi yao hawakuufikia. Muundo wake ulikuwa imara na wa kweli, kiasi kwamba haukuhitaji kuundwa upya na wale waliokuja baada yake.TK 60.5

  Vuguvugu kubwa ambalo Wycliffe alilianzisha ili kuyaweka huru mataifa yaliyokuwa yamekamatwa kwa muda mrefu na Kanisa la Roma chanzo chake kilikuwa katika Biblia. Hapa ndipo chanzo cha chemchemi ya baraka ambayo ilikuwa imetiririka katika kame kadhaa tangu kame ya kumi na nne kilipokuwepo. Huku akiwa ameelimishwa kuheshimu Kanisa la Roma kama mamlaka isiyokosea na kukubali kwa kicho bila maswali, mafundisho na desturi za miaka elfu, Wycliffe aliyapa kisogo haya yote ili asikilize Neno Takatifu la Mungu. Badala ya kanisa kunena kupitia kwa Papa, alitangaza sauti ya Mungu anenaye kupitia kwenye Neno lake kuwa mamlaka pekee ya kweli. Alifundisha pia, kuwa Roho Mtakatifu ndiye mfasiri pekee wa Neno.TK 61.1

  Wycliffe alikuwa mmoja kati ya Wanamatengenezo wakuu. Ni wachache tu waliokuja baada yake waliolingana naye. Usafl wa maisha, bidii isiyokoma katika kujifunza na kufanya kazi, uadilifu usiombuniwa, na upendo ulio kama Wakristo, ni tabia zilizodhihirika kwa Wanamatengenezo wa awali.TK 61.2

  Biblia ndiyo ilimfanya akawa vile alivyokuwa. Kujifunza Biblia kutaadilisha kila wazo, hisia, na shauku kuliko majifunzo mengine yoyote. Inaimarisha nia, inaongeza ujasiri na ustahimilivu. Kama watu wangejifunza Maandiko kwa dhati na unyenyekevu, ulimwengu ungepata watu wenye akili nyingi zaidi, na wenye kanuni za kiungwana zaidi, kuliko zote ambazo zimetokana na majifunzo yanayofikiriwa kuwa bora ambayo falsafa ya mwanadamu imeweza kutoa.TK 61.3

  Wafuasi wa Wycliffe, wanaofahamika kama Wycliffites na Waloladi, walisambaa hadi katika nchi zingine, wakibeba Injili. Wakati huu ambapo kiongozi wao alikuwa ameondolewa, wahubiri hawa walifanya kazi kwa ari zaidi kuliko wakati uliopita. Watu wengi walikusanyika ili kusikiliza. Baadhi ya waliokuwa kati ya waungwana, hata mke wa mfalme, ni baadhi yao walioongoka. Mahali pengi, ishara za ibada za sanamu za Kiroma ziliondolewa toka makanisani.TK 61.4

  Lakini mara, mateso yasiyo na humma yakafumuka kwa wale waliodiriki kukubali Biblia kama kiongozi chao. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Uingereza tamko la adhabu ya kuchomwa moto likatolewa dhidi ya wanafunzi wa Injili. Ufia dini ukafuatiwa na ufia dini. Hali wakiwindwa kama maadui wa kanisa na wasaliti wa ufalme, mawakili wa ukweli waliendelea kuhubiri maeneo yaliyofichika, wakitafuta makazi kwenye nyumba za maskini, na mara kwa mara wakikimbilia hata kwenye matundu na mapango.TK 61.5

  Upinzani uliokuja kwa namna tulivu na yenye uvumilivu dhidi ya upotovu wa imani ya kidini uliendelea kunenwa kwa kame kadhaa. Wakristo wa wakati ule wa awali walikuwa wamejifunza kulipenda Neno la Mungu na hivyo wakateseka kwa uvumilivu kwa sababu yake. Wengi walitoa walivyokuwa navyo kwa ajili ya Kristo. Wale waliopata kibali cha kukaa kwenye nyumba zao waliwahifadhi kwa furaha ndugu zao waliofukuzwa, na wakati wao walipofukuzwa walikubali kwa furaha hali ya kutengwa na jamii. Waliobeba ushuhuda wa ukweli bila hofu hadi kwenye magereza ya chini ardhini na kati ya mateso ya moto hawakuwa wachache, wakishangilia kuwa walionekana kustahili kujua “ushirika wa mateso yake.”TK 62.1

  Chuki ya mamlaka ya Papa haikupozwa na kupumzika kwa mwili wa Wycliffe kaburini. Zaidi ya miaka arobaini baada ya kifo chake mifupa yake ilifukuliwa na kuchomwa hadharani, na majivu yake kutupwa kwenye kijito kilichokuwa karibu. “Kijito hiki,“anasema mwandishi wa kale, “kimepeleka majivu yake hadi Avon, Avon hadi Savem, Savem hadi kwenye bahari ndogo, toka hapo hadi kwenye bahari kuu. Na kwa jinsi hiyo, majivu ya Wycliffe ni kielelezo cha mafundisho yake, ambayo kwa sasa yamesambazwa duniani kote.” 13T Fuller, Church History of Britain, bk. 4, sec. 2, par. 54.TK 62.2

  Kupitia kwa maandishi ya Wycliffe, John Huss wa Bohemia aliongozwa kujitoa toka kwenye makosa mengi ya Uroma. Kutokea Bohemia, kazi ilipanuka hadi nchi zingine. Mkono wa Mungu ulikuwa ukiandaa njia kwa ajili ya Matengenezo makuu.TK 62.3

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents