Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents
Tumaini Kuu - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Sura Ya 36 - Pambano Linalokaribia

    Tangu mwanzo wa pambano kuu mbinguni, limekuwa ni kusudi la Shetani kuipindua sheria ya Mungu. Iwe ni kwa kuitupilia mbali sheria yote ya Mungu, au kwa kupuuzia sehemu ya sheria hizo, matokeo yatakuwa yale yale. Yule ambaye atajikwaa, “katika neno moja” hudhihirisha kukosa juu ya sheria yote; mvuto na kielelezo chake viko upande wa uasi naye atakuwa “amekosa juu ya yote.” Yakobo 2:10.TK 353.1

    Shetani ameyapotosha mafundisho ya Biblia na makosa yameingizwa katika imani ya maelfu ya watu. Pambano kuu la mwisho kati ya ukweli na uongo linahusu sheria ya Mungu, kati ya Biblia na dini ya uongo na mapokeo. Biblia inaweza kufikiwa na wote, lakini ni wachache tu ambao wanaikubali kama mwongozo wa maisha. Ndani ya kanisa wengi wanakana nguzo za imani ya Kikristo. Uumbaji, anguko la mwanadamu, upatanisho, na sheria ya Mungu vimepuuzwa, iwe ni vyote au kwa sehemu. Maelfu ya watu wanaona kuwa kuiamini Biblia ni kuonesha udhaifu.TK 353.2

    Ni rahisi sana kutengeneza sanamu ya nadharia za uongo kama ilivyo kutengeneza sanamu ya mbao au mawe. Kwa kumwasilisha Mungu visivyo, Shetani amewafanya watu wamfikirie Mungu kuwa ni mwenye tabia ya udanganyifu.. Sanamu ya falsafa imeinuliwa na kuwekwa mahali pa Mungu aliye hai kama alivyodhihirishwa katika Neno lake, katika Kristo na katika uumbaji. Mungu huyu wa wanafalsafa, washairi, wanasiasa, waandishi wa habari wengi wa vyuo vikuu vingi na hata baadhi ya taasisi za kiteolojia ni bora kidogo tu kuliko Baali, mungu-jua wa Wafoinike katika siku za Eliya.TK 353.3

    Hakuna kosa linaloshambulia kwa nguvu mamlaka ya mbinguni, hakuna kosa lililo na madhara mabaya kuliko lile fundisho kwamba sheria ya Mungu si sharti tena. Hebu fikiria kama wahubiri maarufu wangefundisha waziwazi kwamba sheria zinazoiongoza nchi siyo za lazima, na kwamba zinazuia uhuru wa watu kwa hiyo hazipaswi kuheshimiwa. Je, ni kwa muda gani watu hao wangevumiliwa kuendelea kuwepo mimbarani?TK 353.4

    Ingekuwa ni sawa kwa mataifa kukomesha sheria zao kuliko Mtawala wa ulimwengu kuiondoa sheria yake. Jaribu la kuiondoa sheria ya Mungu liliwahi kufanyika Ufaransa wakati upagani ulipotawala. Ilidhihirishwa kuwa kutupilia mbali sheria ambazo Mungu ameziweka ni kuukubali utawala wa mfalme wa giza.TK 354.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents